Ilikuwa dakika ya 68 akitokea wing ya kulia baada ya kuwahadaa vyema walinzi wa Mtibwa Sugar na kuiandikia Yanga SC goli la pili na goli la 50 katika rekodi yake na Yanga SC.
Saimoni Msuva aliyezaliwa mwaka 1993 na kujiunga na Yanga SC msimu wa 2013-14 alianza vyema safari yake ndani ya klabu hiyo kongwe nchini akicheza kama kiungo mshambuliaji na winga mahiri wa pembeni.
Katika safari yake ya magoli 50, goli lake la kwanza alifunga dhidi ya URA uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika michuano ya Kombe la Kagame.
Saimoni Msuva mwenye haiba ya upendo , utu na muumini wa umoja klabuni akiongea leo na kurugenzi ya habari ya Yanga SC amesema goli lake la 50 amelitoa zawadi kwa wazazi wake . Wazazi ambao wamekuwa mstari wa mbele kumtia moyo kwenye fani yake hii ya mpira hususani anapokuwa katika wakati mgumu.
Msuva hakusita kutoa shukrani zake za dhati kwa viongozi wa Yanga SC , benchi zima la ufundi , wachezaji wenzake na wapenzi wote wa Yanga SC bila kusahau wadau wa mpira nchini kwa sapoti yao kwake kufikia hapa alipo leo na huko anakokwenda.
Saimoni Msuva anachukizwa na watu wenye nyoyo nyepesi kumtupia lawama pale anapofanya vibaya au kushindwa kutimiza yale wanayotarajia .
" siwezi kuwakataza kusema lakini watambue huu mchezo wa soka una kupanda na kushuka kikubwa ni kusimamia miiko ya soka . Mashabiki lazima wajue si muda wote mchezaji utakuwa bora hivyo waache kutubeza lakini kwangu nahesabu ni changamoto tu"
"nafahamu kiu ya wapenzi wangu ni kuniona mara zote nawapa furaha na mimi na waahidi ilo nikiamimi Mungu atakuwa taa yangu kwenye kufanya hayo"
"msimu huu ni mgumu kwani kweli ushindani ni mkubwa lakini nawaaisi mashabiki wote wa timu yangu bado ubingwa ni wakwetu tena msimu huu"
Saimoni Msuva aliyeibuka mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2014-15 ana imani kubwa klabu yake ya Yanga SC ina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wake endapo umoja utaendelea klabuni na jitihada za wachezaji pamoja na benchi lao la ufundi.
Mwisho winga huyu mahiri nchini anawaasa wachezaji wenzake kutokatishwa tamaa na mashabiki , waandishi wa habari za michezo na wadau wengine wa soka wenye tabia za kuwabeza wachezaji . Kikubwa anawaasa kujitahidi kuimarisha ubora wao na kutomwacha Mungu katika jitihada zao.
Post a Comment