Klabu ya Swansea leo imetangaza kumfukuza kazi kocha Francesco Guidolin na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya USA,Bob Bradley.
Guidolin ambaye amejiunga na Swansea mwezi januari akichukua nafasi ya Garry Monk, amefukuzwa leo ambapo ni siku yake ya kuzaliwa akitimiza umri wa miaka 61.
Swansea imeshinda mechi moja tu katika mechi 7 za ufunguzi za EPL msimu huu na sasa inashika nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi hiyo.
Bob Bradley,58, amekuwa ni Mmarekani wa kwanza kuwa kocha timu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.


Post a Comment