Baloteli ni mmoja kati ya wachezaji watukutu na wenye nidhamu ya mashaka katika ulimwengu wa soka la kimataifa lakini moja ya vitu ambavyo muitaliano huyo mwenye asili ya Afrika anavijali ni kulinda kipaji chake kisipotee. Ilifikia wakati akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu uwezo wa Lionel Messi kama mchezaji bora wa dunia, Mario alikuwa na jibu jepesi tu '' hakuna aliye bora kama yeye ulimwenguni''. Licha ya kauli hii kuhesabika kama kauli ya majigambo na dharau kwa Messi lakini inaonesha ni '' passion '' aliyonayo katika kipaji chake.
Nani asiyeujua utukutu wa Athumani Idd '' Chuji'' katika ubora wake wa kusakata kabumbu eneo la kiungo cha chini? Amewasumbua makocha wengi kwa utovu wa nidhamu lakini daima hawakuwahi kumkatia tamaa na kipaji chake ndio maana mpaka leo anacheza mpira huo ingawa yupo katika magharibi ya soka lake.
Malimi Busungu ni mmoja kati ya washambuliaji wazuri wazawa kuwahi kuibuka miaka ya karibuni katika soka la nchi hii. Ana uwezo mzuri wa kucheza nafasi zote za ushambuliaji kwa mfumo wowote ule wa mwalimu. Mpange kama mshambuliaji wa pembeni au kati atakutendea haki kwa uwezo wake kushambulia kwa kasi na kuachia mashuti ya mbali au kuicheza mipira ya juu( aerial balls ).
Kinda huyu mwenye umri wa miaka 23 ambaye Yanga SC walimsajili msimu wa 2015-16 kutokea Mgambo Shooting ambayo kwa sasa imeshuka daraja, aliweza kuichezea Yanga SC mechi za awali za msimu huo kwa mafanikio makubwa akianzishiwa nje kama '' super sub'' na kuanza kuzikonga nyoyo za wanajangwani. Anakubwa vyema katika mechi ya watani wa jadi mzunguko wa mwisho wa ligi kuu msimu wa 2015-16 akitokea benchi kipindi cha pili baada ya timu hizo kwenda sare ya 0-0 mpaka mapumziko. Busungu aliingia na kuleta uhai katika safu ya ushambuliaji baada ya kumtengenezea pasi nzuri Tambwe na kufunga pia na yeye mwenyewe kufunga.
Tangu mwazo wa msimu huu wa 2016-17 mshambuliaji huyo hajaonekana na kikosi hicho cha mabingwa watetezi Yanga SC na tetesi zilizopo , Busungu ametoweka katika kikosi cha timu hiyo akilaumu benchi hilo la ufundi kumnyima nafasi ya kucheza.
Uchunguzi yakinifu unaonesha mchezaji huyu starehe za Dar es salaam ndio chanzo cha ugomvi wake na benchi la ufundi. Kutofika mazoezini, kuja mazoezini na kushindwa kufanya mazoezi kwa muda wote na wenzie huku nidhamu yake ikiwa kikwazo kikubwa kwa kushindwa kuheshimu viongozi wake ndio chanzo cha ukakasi wote huu.
Mara ya mwisho kwa mchezaji huyu kuonekana na kikosi cha timu hiyo ni pale walipoweka kambi Pemba kujiandaa na pambano la watani wa jadi, Ametoweka kambini na akitafutwa aidha apatikane na kushindwa kupokea simu au simu yake kuzimwa muda wote. Hii ni nidhamu mbaya kwa mchezaji mdogo kama yeye.
Paul Nonga alipoona mabo magumu ndani ya klabu hiyo kwa kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara licha yakuwa na mkataba mrefu na klabu hiyo, hakupitia njia ya mgomo na dharau kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo . Aliandika barua ya maombi kuachiwa akacheze timu ambayo itampa muda mwingi katika kikosi cha kwanza . Licha ya kuandika barua yake lakini bado alihudhuria mazoezi na nidhamu yake ilikuwa nzuri mpaka viongozi wa timu hiyo walipomruhusu kwenda Mwadui FC. Alitambua thamani ya nidhamu yake katika kulinda masilahi yake na kipaji chake.
Benedicto Tinoco amesajiliwa na Yanga msimu wa uliopita ndani ya ligi kuu lakini katika mechi 30 zote za ligi , 6 klabu bingwa na mechi 8 za kombe la shirikisho hakuwhi hata kukaa benchi lakini hakuwa kuonesha utovu wa nidhamu wala ugomvi na viongozi. Kujitambua ni muhimu sana katika fani yako.
Tayari tetesi zimeanza mchezaji huyu anataka kusajiliwa na Majimaji FC wakati wa dirisha dogo linalofunguliwa Novemba 15 hadi Disemba 15. Swali ni moja tu , kwa vimbwanga anavyowafanyia Yanga watakubali kumuuza? au yupo tayari kulipa fidia za kuvunja mkataba?
Wadau wa soka ambao tupo karibu na vijana hawa wadogo katika soka muda mwingine tunashindwa kuwapa ushauri chanya kulinda na kukuza vipaji vyao. Naamini kabisa Busungu anakosa washauri wazuri kuitendea haki kazi yake.
Siamini benchi la ufundi chini ya Hans Van Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi kuwa na kinyongo na kijana huyu kuichezea timu hiyo. Tazama wachezaji waliosajiliwa msimu huu ambao wamepewa nafasi kuitumikia timu hiyo katika kikosi cha kwanza . Vicent Andrew, Hassani Kessy na Mahadhi ingawa kwa sasa anawapisha wenzake katika mzunguko wa kawaida kupeana nafasi kucheza.
Busungu yampasa kuamka usingizi na kutambua thamani ya kipaji chake badala ya kuongozwa na hasira , dharau na mambo mengine ambayo yanaonesha utovu wa nidhamu,


Post a Comment