Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: MTAZAMO WANGU TIMU YA VIJANA YA YANGA SC .
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Samuel Samuel Tatizo la msingi la timu ya vijana ya Yanga SC ni eneo la ushambuliaji.    Nsajigwa amefanikiwa vyema kuijenga timu kweny...

Na Samuel Samuel

Tatizo la msingi la timu ya vijana ya Yanga SC ni eneo la ushambuliaji.
   Nsajigwa amefanikiwa vyema kuijenga timu kwenye backline na eneo la kiungo lakini safu ya ushambuliaji bado.
  Timu inatengeneza nafasi nyingi lakini wanashindwa kuzitumia. Kukosa utulivu na uwezo mdogo kupambana.
  Ni kama mfumo unamzunguka Yusufu Mhilu ambaye akibanwa na kukosa plan B basi timu inajikuta inacheza bila mipango mizuri ya kutafuta goli.
   Kingine wanaonekana kukosa stamina ya kutosha kucheza kwa kasi muda wote . Wanaanza kwa kasi katika mipango mizuri ya kushambulia lakini baada ya muda wanajikuta wanacheza nyuma ya mstari kwa kujilinda na kutegemea counter kufika mbele.
  Mwisho kabisa legacy ya senior timu inawatesa kisaikolojia na kimbinu pia.
  Wanacheza kutembelea ubora wa timu kubwa hii inawafanya kucheza kwa tension kusaka matokeo mazuri na mwisho wa siku kukosa muunganiko mzuri kimbinu .
  Legacy hiyo hiyo inawafanya wapinzani kuwakamia ili kudhihirisha ubora mbele yao kitu ambacho kinamletea ukinzani mkubwa kimbinu na kiufundi Nsajigwa na vijana wake.
  Mwisho niseme wazi ni mwanzo mzuri kwa timu ambayo ina miezi minne tu toka ifanyiwe usajili na kusukwa upya . Hongera uongozi na kocha mkuu Shadrack Nsajigwa .
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top