Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: YANGA SC IMEBAKIZA MKIA TU KUINASA SAINI YA JUSTIN ZULLU TOKA ZESCO UNITED
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ukiingia viunga vya jiji la Lusaka na nchi nzima ya Zambia kwa wadau wa soka na wapenzi wa Zesco United ukatamka jina la Justin Zullu , ni l...

Ukiingia viunga vya jiji la Lusaka na nchi nzima ya Zambia kwa wadau wa soka na wapenzi wa Zesco United ukatamka jina la Justin Zullu , ni lazima upokee tabasamu la aina yake . Ni fahari yao na nguzo muhimu kwao kujivunia.

Kiungo huyu mahiri aliyezaliwa miaka 27 iliyopita ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo jiji la Lusaka , ana urefu wa futi 6 na nchi 1 akiwa na urefu wa kutosha kulihimili eneo la kiungo ambalo ndio limempa sifa zote hizi toka alipoanza kusakata kabumbu akiwa kijana mdogo wa miaka 16 ndani ya National Assemly.

Zullu anaetumia miguu yote anacheza vyema nafasi zote za kiungo ( versatile player ) akivuma sana kama kiungo mkabaji mwenye uwezo wa kukaba , kuanzisha mashambulizi na kuituliza vyema timu inapokuwa inayumba kimbinu kwa kusimamia vyema mfumo wa mwalimu ( skillful ). Uwezo huu ndio uliowafanya mabingwa wa Zambia , Zesco United kumnyakua kiungo huyo toka Kabwe Warriors alikokuwa akitumika kama kiungo mkabaji na kuifanya timu hiyo kuwa moja ya timu nzuri katika eneo la kiungo cha chini.

Alipotua Zesco United 2013 akikutana na George Lwandamina , alikuwa akitumika kama kiungo mkabaji au wakati mwingine kupangwa kama kiungo mchezeshaji wakicheza pamoja na Meshack Chaila ambaye pia ni kiungo tegemeo ndani ya timu hiyo . Muunganiko wao uliwafanya Zesco kunyakua kombe la ligi mfululizo 2014 na 2015 pia kombe la Barclays.

Yanga SC ipo mbioni kumnyakua kiungo huyu ili kuimarisha nafasi yake ya kiungo cha chini . George Lwandamina ( GL ) akiongea na blog yetu Balozi sportsite alisema ; " nimetazama mikanda mbalimbali ya timu yangu mpya nimegundua kuna tatizo kwenye nafasi ya kiungo . Nikimpata Zullu nitakuwa nimemaliza tatizo hilo . Nina mfahamu vyema nikiwa nae Zesco na timu ya taifa hivyo ni kazi rahisi kumpa majukumu na kuyatimiza "

Endapo Yanga itafanikiwa kumnasa mchezaji huyu mwenye uzoefu mkubwa kimataifa akiwa na Zesco United ligi ya mabingwa na timu yake ya taifa , basi watakuwa wamepata mchezaji mzuri kuwabeba katika michuano ya klabu bingwa iliyo mbele yao na mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara unao anza Desemba 17.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top