Winga Gareth Bale yupo katika mbio za kupambana na muda wa kuwa fiti kwa ajili ya mechi ya El Clasico ambapo zimebaki siku 10 pambano hilo kupigwa katika dimba la Camp Nou.
Bale ameumia kifundo cha mguu katika kipindi cha pili kwenye mechi ya jana dhidi ya Sporting Lisbon ambayo mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo ya Klabu bingwa ulaya waliibuka na ushindi wa 2-1.
.
'Bale amepata maumivu ya kifundo cha mguu na yupo kwenye njia mbaya kwa sasa lakini ni mapema sana kusema atakosa El Clasico au hapana,' amesema kocha
Zinedine Zidane baada ya mchezo
Bale alitolewa katika dakika ya 58 ya mchezo huo na nafasi ya kuchukuliwa na Marco Asensio.


Post a Comment