Na S.s
" wanipeni mkataba hawatajutia kazi yangu uwanjani "
Alisema Ankool(Ngasa) alipokuwa akiongea na Balozi sportsite.
Mrisho Khalfan Ngasa amerejea nchini katika mapumziko mafupi akitoa Urabuni katika klabu yake ya Fanja FC aliyoingia nayo mkataba hivi karibuni akitokea nchini Afrika Kusini.
Baada ya kutua nchini na kukuta ligi kuu ipo katika mapumziko mafupi ya dirisha dogo la usajili , Ngasa ameweka wazi kutamani kurudi katika ligi hiyo ambayo imempa umaarufu mkubwa akichezea vilabu vyote vikubwa nchini Yanga SC , Azam FC na Simba SC.
" nipo katika mapumziko lakini kama kuna klabu itahitaji huduma yangu sina pingamizi endapo tu mahitaji yangu yatasikilizwa na mawasiliano mazuri na klabu yangu ya Fanja. Mkataba wangu na wao haunifungi kuuvunja katikati maana tuliwekana wazi katika hilo"
Kiungo mshambuliaji huyu mwenye mapenzi makubwa na Yanga SC anaonesha nia ya dhati kutaka kurudi nchini kwenye ligi ya ushindani kuliko huko aliko ambapo ligi yao bado ipo chini ni kiasi cha kuvuna tu hela za matajiri wa mafuta.
Wakati akivunja mkataba wake na Free Orange State ya nchini Afrika Kusini , alihusishwa kujiunga na mabingwa watetezi nchini Yanga SC lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na kuikuta ligi ikiwa katikati ya mzunguko wa kwanza na tayari benchi la ufundi la klabu hiyo lilikuwa tayari imezipanga vyema hesabu zake kwa vijana 26 wa klabu hiyo.
Ngasa aliambia Balozi sportsite kwamba ; " wengi hudhani mtu akitaka kurudi nyumbani ni amekosea hesabu zake katika soka la kulipwa nje ya nchi , lakini inafika wakati inabidi urudi nyumbani kujipanga upya baada ya kukutana na vitu ambavyo ni kinyume na matarajio yako . "
Gwiji huyu aliyeingia katika soka la ushindani mwaka 2004 akitokea Kagera Sugar na kujiunga rasmi na Yanga SC mwaka 2006 , anahesabika ni mmoja kati ya viungo washambuliaji bora kuwahi kutokea nchini miaka 10 iliyopita akitamba vyema na Yanga SC , Azam FC na kwa uchache na Simba SC pia timu ya taifa ya Tanzania.


Post a Comment