Nchi wanachama wa FIFA wanapangiwa viwango vyao na shirikisho hilo kwa kuzingatia mambo manne yafuatayo;
Kabla ya kuangalia mambo au vigezo hivyo vinne , kwanza tuifahamu formula inayotumika kupata viwango hivyo .
alama zinapatikana kwa ;
a. Alama za matokeo za mechi zilizopo katika kalenda ya FIFA. ( M )
b. Umuhimu wa mechi ( I )
c. Nguvu ya shirikisho la soka timu inapotoka ( T )
d. Nguvu ya timu husika ( kiwango )
Baada ya kuijua formula hiyo muhimu sasa tuangalie vigezo vinne vinavyotumika kupanga viwango ;
Tunaanza na M ( match results ) . Timu ikishinda inapata alama 3, ikitoa sare alama 1 na ikifungwa alama 0.
Tunakuja I ( importance of the match ): hapa alama utolewa kulingana na umuhimu wa mashindano kama ifuatavyo;
a. Mechi za kirafiki FIFA hutoa alama 1.0
b. Mechi za kufuzu kombe la dunia FIFA wanatoa alama 2.5
c. Mashindano chini ya shirikisho la bara husika mfano AFCON au EUROS shirikisho la soka duniani FIFA wanatoa alama 3.0
d. Mechi ndani ya michuano ya kombe la dunia FIFA wanatoa alama 4.0.
Tunakuja alama T kwenye formula yetu ambayo inasimamia nguvu ya mpinzani ( strength of the opponent )= hii inatoa alama 200 kwa bingwa wa dunia na inashuka kwa alama 2 kwa mshindi wa pili. Mfano kwa sasa anaeshikilia namba 1 duniani kwenye msimamo wa FIFA ni Argentina ambaye ukicheza nae na kumfunga unapata alama 200 lakini ukicheza na namba 2 wake ambaye ni Brazil unapata 198.
Tunakuja na herufi C ambayo inasimamia nguvu na kiwango cha shirikisho husika la bara ambapo timu inatoka. Tuangalie alama zao ambapo timu inazipata ikicheza na timu inayotoka katika bara husika.
1. Shirikisho la Ulaya na Amerika kusini wametengewa alama 1.0
2. Amerika kaskazini na kati alama 0.88
3. Afrika na Asia wana alama 0.86.
4. Shirikisho la Oceania 0.85
Ukizidisha vigezo vyote hivyo vinne kwa mechi husika utapata alama za kiwango cha timu husika .
Kadri timu inavyocheza mechi nyingi zilizopo ndani ya kalenda ya FIFA na timu zilizopo juu yake kwa viwango , ubora wa shirikisho inapotoka basi ndivyo inavyopata alama nyingi na kujiweka vyema kwenye viwango vya FIFA.


Post a Comment