Kikosi leo hii kimefanya mazaoezi yake ya mwisho tayari kuwavaa Ndanda Fc hapo kesho kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara mchezo utakaofanyika Uwanaja wa Uhuru.
Akiongea na Balozisportsite baada ya kumaliza mazoezi mwalimu Juma Mwambusi alisema
"Tumejiandaa vyakutosha na wachezaji wapo kwenye hali nzuri na morali yao iko juu kuelekea mchezo wa kesho"
"Kuelekea mchezo huo tuna wachezaji majerui watatu ambao ni Matheo Antony,Beno Kakolanya na Malimi Busungu."
"Tunafahamu kuwa kweli Ndanda ni moja ya timu ambayo huwa inatupa changamoto sana kwenye kupata matokeo ila naamini kwa maandalizi tulioyafanya tutaweza kuchukukua point zote tatu hapo kesho"
Pia mwalimu aliongeza kuwa
"Tunafahamu kuwa matokeo ya mchezo uliopita dhidi ya African lyon yaliwakwaza sana mashabiki wetu lakini ni moja ya matokeo ya kimpira kikubwa ni kuzidi kuipa timu yao sapoti kubwa na bado mbio za ubingwa zipo wazi na tunafahamu kabisa nafasi bado tunayo ya kuutetea ubingwa wetu kwa mara nyingine".
Ndanda tayari wapo jijini na leo hii walikuwa uwanja wa Uhuru wakijiandaa na wao kuelekea mchezo wao dhidi ya Yanga hapo kesho.
Post a Comment