Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: TATHIMINI YANGA SC VS NDANDA FC
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Samuel Samuel Ni moja ya mchezo mzuri katika duru la pili la ligi kuu Tanzania bara. Mara nyingi Ndanda FC na Yanga SC zinapokutana uwa...


Na Samuel Samuel

Ni moja ya mchezo mzuri katika duru la pili la ligi kuu Tanzania bara. Mara nyingi Ndanda FC na Yanga SC zinapokutana uwanjani kunakuwa na hali ya kukamiana sana lakini leo umeonekana mchezo wa kistaarabu ingawa ulikuwa wa upande mmoja.

Kimbinu na kiufundi/ Ndanda FC

Sijui mwalimu Mawazo alikuwa na malengo gani na mechi hii ( game plan ). Ni moja kati ya mechi iliyoonesha udhaifu mkubwa kimbinu na kiufundi kwa upande wa Ndanda. Licha ya kuingia uwanjani kwa mfumo wa 4-4-2 lakini dakika 20 za mwamzo tu walivurugika nakuonekana timu inacheza bila muunganiko sahihi kimbinu na kiufundi. Walihama kutoka 4-4-2 na kuingia 3-6-1 ili kujaribu kuwabana Yanga eneo la kiungo ambapo Makapu na Niyonzima waliwapoteza vilivyo.

Salumu Telela alikosa mipango ya kuiunganisha timu mbele pia kiungo wake nyuma akajikuta muda wote kucheza chini ya mstari hali iliyompa kazi rahisi Juma Makapu kujenga mashambulizi mazuri kwa kupenyeza mipira pembeni ( tactical switching ) kwa Emanuel Martin na Saimoni Msuva.

Nafasi ya ulinzi kwa Ndanda FC hususani walinzi wa pembeni na mawinga wao , walikosa mbinu kabisa kuwazuia Yanga SC kujenga mashambulizi makali kupitia pembeni.  Hii iliwapa mwanya Yanga kutengeneza mashambulizi mengi ya upande .  Goli la kwanza la Yanga limefungwa dakika ya 4 ya mchezo na Donald Ngoma baada ya mpira wa adhabu ya kona . Walinzi wa Ndanda wanamuacha Ngoma anaruka free hii inaonesha uwezo mdogo kwenye marking. Uzembe wa beki ya Ndanda umeipa Yanga goli 3 ndani ya dakika 26 .

Mawazo alionekana kubadilika kipindi cha pili kwa kuweza kupunguza kasi ya Yanga kushambulia kwa kujaribu kuibana Yanga lakini dakika ya 89 makosa yale yale kwa kushindwa kufanya marking Bossou kwenye kona anaruka free na kuandika bao la nne.

Kimbinu na kiufundi/ Yanga SC

George Lwandamina amezichanga vyema karata zake kimbinu na kiufundi kwa kuanza na mfumo ambao umempa muunganiko mzuri katika mbinu za ulinzi na kushambulia.

Ameiingiza timu uwanja kwa 4-4-2 lakini akilenga kushambulia kutokea pembeni akiwabana Ndanda kwa kutumia viungo wawili tu Juma Makapu na Haruna Niyonzima .

Kushoto alimweka Emanuel Martin ingizo jipya toka JKU akilenga vitu viwili . Kwanza kasi na nguvu zake kuwarudisha nyuma wachezaji wa Ndanda ili kuvunja " striking force " pembeni . Martin amecheza vyema kama mshambuliaji wa pembeni lakini wakati huo huo akitumika kutengeneza krosi kwa Tambwe na Ngoma kama winger . Alichofanikiwa ni kuwasiliana vyema na Haji Mwinyi wakati wa kupanda na kushuka na pia kufanya switching na Makapu ili kupokea mipira inayotokea kati .

Msuva kulia leo hakuwa kwenye mchezo mzuri sana katika kupanda lakini Lwandamina alipata faida ya mchezo mzuri kwa beki wake wa kulia Juma Abdul . Alikuwa vyema kupanda na kutengeneza krosi nzuri wakati huo huo akimlinda vyema Dida kulia.

Mbinu za ulinzi za Lwandamina zilianzia kati kwa Juma Makapu . Amezidi kumwamini kama kiungo mkabaji lakini kazi kubwa akimpanga kuvunja mipango ya wapinzani kati na kusambaza mipira kulia na kushoto. Wengi wanajiuliza kwanini hapeleki mipira mbele kupitia kati ( direct play ) . Makapu ni deep lying holding midfielder. Ni aina ya viungo wakabaji wanaocheza kuimarisha ulinzi chini ya mstari wa mashambulizi lakini wakipangiwa kiungo wa juu mwenye " free role task " . Kiungo anacheza huru kama box to box midfielder ambaye huyu sasa ndio anatengeneza daraja kati ya kiungo na ushambuliaji kupitia kati . Hii ndio ilikuwa kazi ya Haruna Niyonzima leo kabla ya kuingia Kamusoko na chini yake Justin Zullu.

Zullu vs Makapu

Dakika 35 tu zimetosha kuonesha tofauti ya Juma Makapu na Justin Zullu . Kwanza kabisa kimbinu na kiufundi , Lwandamina amelamba joka hapa . Makapu anakupa huduma yake kwenye mechi inayohitaji vita ya viungo . Mechi inayohitaji timu kutawala eneo la kiungo kwa kuwatoa wapinzani mchezoni ( cut off/ blocking & switching) . Ndanda leo walipoteq kati kwa ubabe wa kiungo huyu lakini pia akiwaunganisha Yondani na Bossou nyuma yake ( masking ). Lakini alihitaji msaada wa Niyonzima pale timu ilipohitaji kupita kati .

Zullu si kiungo mkabaji anaekaa chini ( deep lying holding midfielder) huyu ni kiungo mkabaji asilia anaeiunganisha timu nyuma na mbele .( defensive midfielder) . Zullu anapiga pasi fupi na ndefu mbele . Ahitaji kiungo mchezeshaji ili kuwafikia washambuliaji . Hii kimbinu ina maana anakupa faida mwalimu kiungo wako namba nane kugeuka kiungo mshambuliaji kificho kwa kupokea pasi za mwisho toka kwake . Ingawa bado anaonekana bado hayupo fit kifiziki.

Asanteni .

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top