Fahamu kiasi cha pesa itakachopata Yanga ikiwa itaingia katika hatua ya makundi klabu bingwa Africa 2017.
Kuanzia mwaka 2017 michuano ya klabu bingwa itajulikana kama TOTAL CAF CLUB CHAMPIONSHIP...chini ya udhamini wa kampuni ya TOTAL zifuatazo ndizo zawadi kwa washindi mbali mbali.
Ikiwa Yanga itafika katika hatua ya makundi na kushika nafasi ya mwisho au ya tatu katika kundi itajipatia kiasi cha dola za kimarekani 550,000 sawa na Tsh bilioni moja na milioni 100 ikiwa tu exchange rate ni TSH 2000 = USD 1.
Yanga ikifanikiwa kushika nafasi ya kwanza au ya pili katika kundi na kuingia robo fainali basi itajipatia kiasi cha dola za kimarekani 650,000 sawa na bilioni moja na milioni 300 (ikiwa tu exchange rate ni 2000 TSH=USD 1)
Yanga ikifanikiwa kuvuka hatua ya robo fainali na kuingia nusu fainali basi itajipatia dola za kimarekani laki nane sawa na bilioni moja na milioni 600 tsh(ikiwa exchange rate ni USD 1=TSH 2000)
Ikiwa Yanga itavuka hatua hiyo na kuingia fainali ,kama itakua mshindi wa pili kwa maana ya kushindwa fainali basi itapata kiasi cha dola za kimarekani milioni moja na laki mbili na nusu(USD 1,250,000) ambazo ni sawa na tsh bilioni mbili na milioni mia tano( ikiwa tu exchange rate ni USD 1=2000 TSH)
Ikiwa Yanga watakua mabingwa basi watapata dola za kimarekani milioni mbili na laki tano sawa na tsh bilioni tano (ikiwa exchange rateUSD 1=2000 Tsh)
Lakini pia katika kila hiyo hatua Shirikisho la Soka Nchini pia litakua likipata zawadi kulingana na hatua timu itakayofikia kama ifuatavyo
Hatua ya makundi TFF watapata USD 27,500 sawa na TSH milioni 55.
Hatua ya robo fainali TFF watapata USD 32,500 sawa na TSH milioni 65.
Hatua ya nusu fainali TFF watapata USD 40,000 sawa na TSH milioni 80.
Mshindi wa pili, TFF watapata USD 62,500 sawa na TSH milioni 125.
Bingwa, TFF watapata USD 125,000 sawa na TSH milioni 250.
Mapato haya hayahusishi gate collection ambazo Timu na Shirikisho watakua wakipata kwa mechi zitakazokua zinapigwa uwanja wa Taifa.
Hakika ni mda wa kubadiri mitazamo yetu kuhusu soka la ridhaa na turuhusu soka la kulipwa ili kupata wawekezaji zaidi katika soka letu tuweze kua na ushindani sahihi ,huwezi kugombea bilioni tano kwa kikosi cha milioni 100, wachezaji bora wote ni ghali kuwapata tuamke sasa mpira ni biashara.
Jitahid babu kutupa habari mpya kila siku unakaaga kimya sana
ReplyDeletehabari zako nazikubali sana huwa zinauhakika asilimia