Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: ZLATAN: RONALDO DE LIMA NI BORA KULIKO CRISTIANO RONALDO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katika mahojiano ya hivi karibu aliyofanyiwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na kituo cha ESPN Brazil, aliulizwa kuwafananisha watupiaji wa ...

Katika mahojiano ya hivi karibu aliyofanyiwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na kituo cha ESPN Brazil, aliulizwa kuwafananisha watupiaji wa magoli wawili, Ronaldo De Lima na Cristiano Ronaldo. Kama kawaida yake, hakuogopa kuongea kilichopo katika fikra zake.
.
'Ninafikiri Ronaldo,II Fenomeno alikuwa bora. Alikuwa ni mfano wa kuonesha mpira wa miguu ukoje. Kila kitu alichofanya ilikuwa "Wow" . Jinsi alivyokuwa anakokota mpira, jinsi alivyokuwa anakimbia.

Ronaldo alikuwa asilia (Natural). Alizaliwa kuwa alivyokuwa. Haikuwa kitu cha yeye kujifunza kuwa vile.Mchezaji wa aina hii hatengenezwi,anazaliwa. Ni wa kipekee.'
.

Kuhusu Cristiano Ronaldo, Zlatan alisema " Ni tofauti kwa Sababu yeye (Cristiano) ni matokeo ya mazoezi magumu. Si asilia (Not natural).

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top