Mabingwa wa tetezi wa kombe la mapinduzi URA leo hii wameibuka kidedea baada ya kushinda mchezo wao wa kwanza.
Mchezo huo ulikuwa wa kushambuliana kwa pande zote mbili.
Mpira mpaka kipindi cha kwanza kinaisha milango yote miwili ilikuwa migumu kwani hakuna aliekuwa ameweza kuona lango la mwenzie.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana na URA waliweza jipatia goli la kuongoza kupitia kwa Labama Bokota kwenye dakika ya 57 ya mchezo.
Timu zote mbili zilifanya mabadiliko ambao kwa upande wa URA yaliweza kuzaa matunda kwani zikiwa zimebakia dk 1 mpira kumalizika waliweza jipatia goli la pili kupitia kwa yule yule Labama Bokota na kuifanya URA kujiakikishia ushindi wao wa kwanza.
"Mchezo ulikuwa mgumu sema vijana wangu walijitaidi na kama mlivyoona tumeweza kuibuka na ushindi na tumekuja hapa kwaajili ya kutetea tu ubingwa wetu kwa mara nyingine tena"
Hayo ni maneno ya Mwalimu wa URA baada ya mchezo kumalizika.
Post a Comment