Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: SIMBA SC YASHINDWA KUKAA KILELENI KUNDI A
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mashindano ya kombe la mapinduzi yameendelea tena siku leo hii kwa kuchezwa michezo miwili. Mchezo wa kwanza ulikuwa jioni ya saa 10 ambao ...

Mashindano ya kombe la mapinduzi yameendelea tena siku leo hii kwa kuchezwa michezo miwili.

Mchezo wa kwanza ulikuwa jioni ya saa 10 ambao tuliweza kuona mabingwa watetezi wakiwasambaratisha  timu ya KVZ kwa magoli mawili kwa bila.

Mchezo wa usiku ambao ndio mchezo wa pili kwa siku ya leo ambapo Simba walikuwa wakucheza na Taifa Jang'ombe.

Mchezo huu ulikuwa wakusisimua sana na wenye uvutani kwa pande zote mbili.

Simba walijipatia goli la kuongiza dk ya 28 kupitia kwa Mzamiru Yasini,haikuchuichukua muda mrefu sana zikiwa zimesalia dakika takribani nne kufika mapumziko kupitia kwa Juma luzio simba wakaongeza goli lingine ambalo lilipelekea simba kuongoza kwa magoli mawili kwa bila mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana timu zote mbili zilifanya mabadiliko ambayo yalifanya mpira kubadilika kwa kiasi kikubwa tofauti na kipindi cha kwanza cha mchezo.
Ilikuwa ni dk ya 76 Lufungo alijifunga goli na kuwafanya taifa Jang'ombe kurudi mchezoni wakifanya mashambulizi mengi langoni mwa Simba.

Mpira ulimalika kwa matokeo kusalia hayo hayo 2-1 nakuifanya Simba kujizolea point tatu muimu na kuwa wapili kwenye kundi A nyuma ya vinara URA ambao wao wana point tatu na magoli mawili na hawajafungwa goli ata moja.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top