Na Ally Kamwe
Kwanza sote tunatakiwa kufahamu kuwa Mkhitaryan alifunga akiwa ‘offside’ na Giroud alifunga akiwa ‘Onside’. (Tuumeze kwanza huu ukweli mchungu kisha tuendelee na mjadala.
Ni kweli Mkhitaryan alifaidika na ile ‘offside’? Ndio, kivipi? Tuanzie hapa.
Kitendo cha kuwa mbele kidogo ya mabeki wawili wa Sunderland (ambao pia hawakuruka) kilimpa Mkhitaryan nafasi nzuri zaidi ya kuiona pasi ya Ibrahimovic na kufanya maamuzi ya namna ya kuupiga mpira kwa staili ile.
Giroud alifunga bao lile mbele ya Kiungo wa Crystal Palace, Flamini (aliyesimama nae kwenye mstari mmoja, ‘Onside position’) na kibaya zaidi Flamini aliruka katika jitihada za kuizuia krosi ya Sanchez.
Kwanini tunatakiwa kumsifia Giroud katika hili?
Alikuwa na ‘timing’ nzuri kichwani mwake. Pasi ilipigwa nyuma na tayari kulikuwa na Flamini ambaye alimkinga lakini bado alichekecha kichwa chake na kuinua mguu na kuupiga mpira.
(Huenda ni bahati kama alivyosema, lakini kitendo tu cha kuupigia hesabu ile krosi ya Sanchez, OG anastahili sifa kwa hesabu zake.
Umejifunza nini mpaka hapa?
Giroud alifunga bao bora katika mazingira magumu zaidi kuliko Mkhitaryan (japo yote ni mabao bora)
Turudi nyuma kidogo na tuangalia mazingira ya kimchezo yalivyokuwa hadi kupatikana kwa mabao haya, tuanze na Mkhitaryan.
Mpaka Mkhitaryan anafunga bao lile (dakika ya 84) United walikuwa mbele kwa bao 2-0. Katika hali ya kawaida kabisa, akili za wachezaji wa Sunderland zilishatoka mchezoni, ni kama walishakubali kichapo pale Old Trafford.
Wakajiachia na wakaifanya United icheze kwa nafasi, tazama;
Valencia aliyepiga pasi kwa Ibra (hakukabwa na mtu)
Ibra aliyepiga pasi kwa Mkhitaryan (Hakukabwa na mtu)
Mkhitaryan aliyefunga (Alikuwa katikati ya mabeki wanne ambao hamna hata mmoja aliyemfanyia ‘marking’ kama mtu hatari kwenye eneo lao hatari)
Kati hali hii ya kimchezo, ilikuwa rahisi zaidi kwa Mkhitaryan kufunga bao lile kwa ubora ule.
Mtazame Olivier Giroud.
Kwanza alilifunga dhidi ya Crysta Palace iliyo chini ya Big Sam. ( Morali yao imebadilika sasa, wanacheza kwa kupambana sana ili kukwepa kushuka daraja, kiuchezaji wanaonekana tofauti kabisa na Sunderland)
Hivyo mpaka dakika ya 17 walipofungwa bao lile, asilimia 90 ya akili za wachezaji bado zilikuwa zikipambana kwa ajili ya kutafuta pointi pale Emirates.
Tazama mazingira ya bao, ‘move’ ilikuwa ni ‘counter attack’ (shambulizi la kushtukiza).
Zilipigwa pasi 4 kabla ya bao (lakini tusisahau kuwa Giroud ndiye aliyepiga pasi ya pili, akiwa zaidi ya mita 50 na lilipo lango la Palace).
Giroud alikimbia toka katikati ya uwanja kwa kasi kabla ya kufunga bao lile (Ni tofauti na mazingira ya bao la Mkhitaryan)
Kwangu, bao la Mkhitaryan ni bora lakini lile la OLIVIER GIROUD ni bora zaidi.
Ahsanteni


Post a Comment