Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: BACARY SAGNA APIGWA FAINI NA FA .
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Chama cha soka cha England FA leo kimempiga faini ya pauni 40,000 beki wa Man City Bacary Sagna kwa alichopost katika akaunti yake ya Instag...

Chama cha soka cha England FA leo kimempiga faini ya pauni 40,000 beki wa Man City Bacary Sagna kwa alichopost katika akaunti yake ya Instagram baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Burnley Jan,2,2017.

Kunako dakika ya 32 ya mechi hiyo City walipunguzwa na kubaki 10 uwanjani baada ya mwamuzi Lee Mason kumpa kadi nyekundu kiungo Fernandinho.

Baada ya mechi hiyo Sagna alipost katika ukurasa wake wa Instagram " 10 against 12... but still fighting and winning as a team". Baada ya muda mchache akaifuta Post hiyo.

Taarifa kutoka FA inaripoti kuwa mchezaji huyo amepata adhabu hiyo kwa maoni yake ya kuuliza/Kuhoji ukamilifu/uaminifu/utimilifu wa maafisa wa mchezo au kudai/kuashiria kuna upendeleo kutoka kwa maafisa wa mchezo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top