Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: SHIRIKISHO LA MPIRA CHINA ( CFA ) LATOA TAMKO JIPYA.....
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
-Leo shirikisho la soka la china CFA limefanya mabadiliko kwenye regulations zao za kuendesha ligi ya kwao. Kuanzia sasa wachezaji wa kigeni...

-Leo shirikisho la soka la china CFA limefanya mabadiliko kwenye regulations zao za kuendesha ligi ya kwao. Kuanzia sasa wachezaji wa kigeni kusajiliwa mwisho 5 tu kwenye timu. Na kwenye 11 wanaoanza , wachezaji 3 tu wa kigeni kucheza  na lazima kuwepo na mchezaji angalau mmoja  wa chini ya umri wa miaka  23 kwenye timu inayoanza mzawa.
  Shirikisho hilo limetoa mabadiliko hayo kuokoa mustakabali wa soka la nchi hiyo hususani ngazi ya timu ya taifa kwa kuweka misingi mizuri ya kutumia wazawa .
  Hivi karibuni vilabu vya soka nchini China vimekuwa vikisajili wachezaji wengi nguli wanaovuma katika ligi kubwa barani Ulaya ili kuimarisha soka lao lakini lengo kubwa likionekana kuwa na mvuto mkubwa wa kibiashara kwa majina makubwa ya soka yanayovuma Ulaya . Hali hii imelifanya shirikisho la soka nchini humo kuweka misingi mapema ili wasije kuchelewa baadae na kujikuta wana ligi bora na yenye mvuto lakini wakiwa hawana msingi mzuri wa soka ngazi ya wazawa kuziimarisha timu zao za taifa na soka kwa ujumla nchini humo .

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top