Klabu ya Barcelona imetangaza kuwa wachezaji wake hawatahudhuria sherehe za ugawaji wa tuzo za FIFA (The Best FIFA Football Awards 2016) zitakazofanyika leo mjini Zurich.
Taarifa kutoka klabuni hapo imesema kuwa wamefikia maamuzi yao kwa sababu ya maandalizi ya mechi yao ya marudiano ya Copa del Rey jumatano hii dhidi ya Athletic Bilbao.
Luis Enrique ambaye nae hapo awali alikuwepo katika kuwania tuzo ya kocha bora kabla ya watatu bora kutangazwa, pia hatahudhuria tuzo hizo.
Katika kuziba nafasi hizo, Raisi wa Barcelona Josep Maria Bartomeu, makamu wa Raisi Jordi Mestre na wajumbe wa bodi kama vile Silvio Elias and Oscar Grau, Albert Soler, Robert Fernandez na Raul Sanllehi watahudhuria.
Post a Comment