1. Saimoni Msuva ( Yanga )
Ameibuka mfungaji bora kwa michuano hiyo akitupia goli 4 . Kubwa kwake ni amezidi kushikiria rekodi ya winga mwenye kasi zaidi nchini na pia kwenye michuano hiyo . Amechangia zaidi ya asilimia 50 kwa timu yake kutinga nusu fainali.
2. Abdullah Haji ( Taifa Jang'ombe )
Nahodha na mlinzi wa kati wa wababe hawa wa Zanzibar. Mechi zote alizocheza alionekana muhimili kamili wa timu yake katika ulinzi pia kusimama kama kiongozi kwa wenzake uwanjani.
3. Abdul Kassim ( Jang'ombe Boys )
Ndio mchezaji wa kwanza kupiga hat trick katika michuano hii mwaka huu . Ana kasi nzuri katika safu ya ushambuliaji na uwezo mzuri wa kumiliki mpira . Aliwatungua KVZ 3 wakipata moja .
4. James Kotei ( Simba SC )
Kiungo Simba SC . Mechi zote alizocheza ameonesha ni nguzo muhimu kwenye klabu hiyo katika nafasi ya kiungo . Licha ya ugeni katika klabu hiyo lakini ameonesha kuelewana vyema na wenzake . Ana uwezo mkubwa kukaba , kusambaza mipira na ku hold mpira pale timu inapopotea kimipango na kuwarudisha wenzake mchezoni.
5. Method Mwanjale ( Simba SC )⚽
Ni kama katokea kwenye Academy za Simba SC kwa uzalendo anao uonesha dhidi ya timu hiyo licha ya ugeni wake . Naweza sema baada ya kuondoka Owino sasa klabu hiyo imepata mbadala wake . Ni mlinzi aliyekamilika kila idara .
6. Yahya Mohamed ( Azam FC )
Sasa wanaweza kumsahau Kipre Tcheche . Yahya ni mshambuliaji mzuri namba mbili nyuma ya John Bocco . Wametengeneza kombinesheni nzuri kwa muda mfupi wakipata back up nzuri ya Joseph Mahundi nyuma yao kushoto . Kasi yao katika kushambulia ni mwiba mkali kwa wapinzani. Yahya ana uwezo mzuri kucheza kama play maker wa juu kutengeneza muunganiko mzuri na viungo .
7. Labama Bogota ( URA )
Licha ya timu yake kushindwa kufika mbali katika michuano hii, mshambuliaji huyu wa kati anaevaa jezi namba tisa alikuwa mwiba mkali kwa wapinzani . Anaondoka Zanzibar na goli mbili lakini akiacha gumzo kwa uwezo wake wa kucheza vyema mipira yote juu na chini na kubwa kwake ni uwezo wa kuvunja mtego wa kuotea.
8. Frank Raymond Domayo ( Azam FC )
Amezaliwa upya?! Hapana ameudhihirishia umma wa wanasoka Tanzania kwamba yeye bado ni chumvi , kiungo muhimu kwenye chakula . Uwezo wake mkubwa wa kumiliki eneo la kiungo umeifanya Azam kutulia vyema eneo hilo akishirikiana vyema na wenzake Sure boy , Stephan na Himidi Mao Mkami " Ninja ". Uwezo wa kupiga mashuti makali na pasi zake zenye macho ni gumzo.
9. Janvier Besala Bokungu ( Simba SC )
Anasimama kama beki bora namba mbili kwenye michuano hii kwa mtazamo wangu . Mashindano haya yamegeuza taswira yake kwa watanzania wenye nyoyo nyepesi za kuhukumu kabla ya kutoa muda wa kuchunguza . Wengi walidharau usajili wake lakini michuano ya Mapinduzi imeonesha uwezo wake kamili katika nafasi hiyo.
10. Saidi Juma " Makapu " ( Yanga SC )
Michuano hii imemfanya aonekana " lulu " Jangwani . Heko kwa kocha Lwandamina kumwamini na kumuongezea ujuzi kuicheza nafasi hiyo . Ameonesha ukomavu na uwezo mkubwa kukimudu kiungo cha chini . Ameingia kwenye mizani ya kupima uwezo wake na kiungo mgeni toka Zimbabwe Justin Zullu .
11. Saidi Mohamedi " messi " ( Jang'ombe Boys )
Amechaguliwa kama mchezaji bora chipukizi kwa uwezo wake kama kiungo mshambuliaji.
* Upande wa makocha ;
1. Idd Nassoro Cheche anashika namba moja akifuatiwa na kocha wa Taifa Jang'ombe.
* mzee Mfaume ameibuka mwamuzi bora wa mashindano akifuata sheria 17 za FIFA pasipo mawaa . Anatoa changamoto njema katika kada hiyo kusimamia weledi wa kazi hiyo ya uamuzi
Post a Comment