Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: PESA ZA CHINA ZALETA VITA CHELSEA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Diego Costa ameachwa katika kikosi cha Chelsea kitachoivaa Leicester leo baada ya kutokea msululu wa kutoelewana na kocha Antonio Conte Ms...

Diego Costa ameachwa katika kikosi cha Chelsea kitachoivaa Leicester leo baada ya kutokea msululu wa kutoelewana na kocha Antonio Conte

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania ,28,anadai kuwa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo lakini timu ya utabibu ya Chelsea hawajakubaliana na madai yake.

Ripoti zinasema kuwa, Costa hajafanya mazoezi na kikosi cha Conte kwa siku 3 zilizopita baada ya kupata ofa ya timu moja ya ligi kuu ya Uchina ambayo itamlipa kiasi cha pauni milioni 30 kwa mwaka.

Imeripotiwa kuwa mchezaji huyo amekuwa hatulii tangu apate ofa hiyo itakayomfanya awe moja ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa duniani, na akaingia katika majibizano na makocha wawili wa mazoezi wa Chelsea na baadaye Conte kuingilia kati, kutokana na taarifa ya Sky in Italy, mwishoni mwa majibizano hayo Conte akambwatukia Costa " Go to China " .

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top