Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: YANGA SC SAFARINI SONGEA KESHO . WATANO KUBAKI JIJINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha Yanga SC kesho alfajiri kitaondoka jijini Dar es salaam kuelekea Songea kuivaa Majimaji FC katika mchezo wa raundi ya 18 wa ligi ...

Kikosi cha Yanga SC kesho alfajiri kitaondoka jijini Dar es salaam kuelekea Songea kuivaa Majimaji FC katika mchezo wa raundi ya 18 wa ligi kuu Tanzania bara.

Mchezo kati ya Majimaji na Yanga SC utachezwa tarehe 17 January.

Yanga inaondoka kesho na msafara wa watu 30 .Wachezaji 21 na viongozi 9 .

Katika mchezo huo kocha mkuu wa Yanga SC , George Lwandamina amethibitisha atawakosa wachezaji watano! Kwa sababu mbalimbali.

Donald Dombo Ngoma anaikosa mechi hiyo kutokana na majeraha ya goti sambamba na Malimi Busungu, Obrey Chirwa na Justin Zullu.

Emanuel Martin anakamilisha idadi ya wachezaji watano kuukosa mchezo huo baada ya kupatwa na msiba nyumbani kwao.

Benchi la ufundi limejinadi kushinda mchezo huo katika harakati za kupunguza gape la pointi na vinara wa ligi Simba SC .  Yanga wanashika nafasi ya pili katika ligi kwa  pointi 40 huku Simba wakiwa kileleni kwa pointi 44.

" kikosi kinasumbuliwa na Majeruhi lakini waliopo watafanya kazi na tumewaandaa vyema kushinda mchezo huo ugenini. " alijinadi kocha msaidizi wa klabu hiyo Juma Mwambusi akiongea na Balozisportsite mara baada ya mazoezi leo hii.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top