Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: MTIHANI KWA OMOG LEO SIMBA SC VS URA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Samuel Samuel Simba SC leo kuwavaa wakusanya kodi wa Uganda URA ( Uganda Revenue Authority) katika mchezo wao wa tatu katika michuano ya k...

Samuel Samuel

Simba SC leo kuwavaa wakusanya kodi wa Uganda URA ( Uganda Revenue Authority) katika mchezo wao wa tatu katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani.

URA ni moja ya timu bora katika michuano hiyo inayocheza soka la uhakika na  ni miongoni mwa timu ambazo zinapigiwa upatu kuondoka na kombe hilo wakiwa kama mabingwa watetezi .

URA walianza michuano hiyo kwa mkwara baada ya kuibamiza KVZ 2-0 mshambuliaji wao Labama akitupia kwenye kamba goli zote mbili.

Taifa Jang'ombe waliwashangaza waganda hao kwa kuwabamiza 2-1 mechi iliyofuata. Licha ya kufungwa lakini ni timu inayoonesha mpira mzuri wa malengo hivyo Simba wajiandae kwa upinzani mkali.

Simba SC waliianza safari ya Mapinduzi kwa kushinda 2-1 dhidi ya Taifa Jang'ombe na mechi ya pili kushinda goli 1-0 dhidi ya KVZ.

Toka vinara hao wa ligi kuu Tanzania bara waingie mjini Zanzibar, licha ya kushinda mechi mbili mfululizo lakini wamekuwa wakionesha udhaifu wa kutumia nafasi nyingi wanazozitengeneza .

Simba imekuwa ikishindwa kucheza kwa kasi muda wote na kuonesha muunganiko mzuri wa safu ya kiungo na ushambuliaji . Hii kimbinu inaonesha bado benchi la ufundi la klabu hiyo halijaonesha kiwango mujarabu kuwanoa washambuliaji wao .

Muzamiru Yassin amegeuka lulu kwenye kikosi hicho licha ya kutokea nafasi ya kiungo lakini ndio mwiba mkali kwa wapinzani . Huyu ndio angalau ana " compose " mipango ya mwalimu katika ushambuliaji. Katika magoli matatu ambayo Simba wameshinda katika michuano hiyo yeye ametupia goli mbili na moja likifungwa na Mohamedi Ibrahimu.

Omog atakuwa na mtihani leo kucheza na timu yenye uzoefu mkubwa na yenye malengo makubwa ya ushindani .

Muhimili wa Simba SC kimbinu umekijikita kwenye nafasi ya kiungo inayoundwa na James Kotei na Jonasi Mkude , URA ni wazuri kimbinu kuwagawa wapinzani kwenye nafasi hii. Hivyo Simba SC wanatakiwa kuwa makini katika hili .

Wengi wamekuwa wakiitabiria Simba kupata upinzani mkali endapo watakutana na timu yenye uwezo mzuri kuwatawanya kwenye safu yao ya kiungo, Stamina na kutengeneza pressure kubwa ya mashambulizi . Simba wategemee upinzani leo katika hili kwa mechi mbili nilizowaona URA wanaliweza hili.

Omog aachane na mbinu za pasi nyingi eneo la kati na awarudishe Simba SC kwenye soka lao la moja kwa moja ( direct play ) . Soka la pasi fupi za kasi zinazoisukuma timu mbele kwa kasi ndio atawaweza Waganda hawa . Jang'ombe walitumia mbinu hii wakawalaza 2-1.

Natamani kumuona Blagnon akianza mechi hii akizungukwa kushoto na MO Ibrahimu, kulia Kichuya Mzamiru na Mkude wakianza kati . Si mbaya Kotei akianzia nje ili kuja kubadilisha mchezo kama sub kwa Mzamiru au Mkude .

Hawa wanauwezo mchezo wa kasi , nguvu na ufundi mwingi wakitengeneza pressure pande zote . Kwa vipaji vilivyopo Simba si timu ya kukosa uwiano kimbinu kutoka safu ya kiungo na ushambuliaji .

Kiu ya kutetea ubingwa na kupoteza mchezo uliopita , itawafanya URA kuingia uwanjani kama bogo aliyejeruhiwa . Tutarajie ushindani mkali .

Mechi nzuri hii.

Asanteni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top