Chama cha soka cha England FA leo kimetangaza kuifuta kadi nyekundu aliyopewa kiungo wa West Ham, Sofiane Feghouli katika mechi ya juzi jumatatu,jan 2 dhidi ya Manchester United.
Maamuzi hayo yamekuja mara baada ya West Ham kukata rufaa kupinga kadi hiyo aliyopewa kiungo huyo kutoka Algeria.
Feghouli alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi Mike Dean katika dakika 15 ya mchezo baada ya kuonekana kumchezea madhambi beki Phil Jones.
Baada ya maamuzi hayo, sasa kiungo yuko huru kucheza mechi ya FA raundi ya 3 ijumaa hii dhidi ya Man City.


Post a Comment