Na Samuel Samuel
Mabingwa watetezi ligi kuu Tanzania bara wameibuka na ushindi wa pili leo katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Unguja. Yanga SC wameitandika Zimamoto goli 2-0 zikitiwa kambani na kiungo mshambuliaji Saimoni Msuva.
Goli la kwanza la Yanga SC lilifungwa dakika ya 11 ya mchezo baada ya faulo nzuri iliyochongwa na timu kapteni Haruna Niyonzima na Msuva kuutokea mpira na kuubetua kwa mguu wa kulia na kutinga nyavuni.
Goli la pili lilifungwa pia na Saimoni Msuva akionesha juhudi binafsi kwa kuwatoka walinzi wa kati wa Zimamoto baada pasi murua ya Thabani Kamusoko na kumchambua vyema golikipa wa Zimamoto na kuipatia timu yake goli la pili dakika ya 21.
Dakika ya 69 Yanga SC walipata penati lakini Saimoni Msuva alishindwa kuipatia goli timu yake baada ya golikipa wa Zimamoto kuucheza mpira.
Kimbinu na kiufundi
Zimamoto SC
Ni msifu mwalimu wa Zimamoto licha ya timu yake kupoteza mchezo huu ukiwa mchezo wa pili mfululizo, lakini timu yake imeonesha mabadiliko makubwa kimbinu kuliko mechi ya awali waliyofungwa 1-0 na Azam FC.
Waliwajua Yanga SC ni wazuri katika nafasi ya kiungo na mwalimu wao George Lwandamina amekuja na mbinu za " Total football " yaani kila mchezaji kuzijua vyema nafasi zote za uwanjani . Mbinu ambazo huimarishwa kuanzia kwa kati kwa viungo wa kati kuhakikisha wanaipanga timu vyema katika mashambulizi na ulinzi kulinda tempo ya timu. Hii inawapa fursa wachezaji wengine kuzunguka uwanja mzima lakini muhimili ukiwa kati.
Zimamoto waliingia na 4-5-1 lakini si kwa mfumo wa kujilinda muda wote . Walijaa kati kuufinya uwanja ili Yanga SC wakose utulivu wa kupanga mashambulizi yao ya kueleweka .
Musa mwingi walikuwa wakivunja mawasiliano ya Zullu na viungo wenzake kwa kumkaba kabla na akiwa na mpira sema ni uwezo binafsi wa kiungo huyo kutamba na dimba zima ulikuwa unawafanya wakati mwingine kushindwa kumzuia kupiga pasi zake nzuri ndefu au kupokea mipira toka kwa walinzi wa kati na kuitafutia safari mbele .
Mchezo wa kuotea ilikuwa ni mbinu nyingine kwa Zimamoto kuua mashambulizi ya Yanga ingawa kasi ya Saimoni Msuva iliwashinda na muda mwingi alikuwa akiua mtego huo hususani goli la pili.
Kukosa mtu makini wa kumalizia nafasi chache walizotengeneza Zimamoto kumewanyima goli lakini pia uvivu wa kupiga mashuti ya mbali kwenye mbinu zao za kuishitukiza Yanga kuliwafanya juhudi zao zote kutozaa matunda . Mata nyingi walikuwa wanajaribu mipira mirefu ya juu ambayo Andrew Vicent imemfanya kung'ara leo kwa kuicheza.
Yanga SC
Kwa mtazamo wa haraka haraka utaona kama haukuwa mchezo wa kimbinu na kiufundi kwa maana ya mipango mizuri ya mwalimu kusaka ushindi bali ilikuwa mechi ya kutazama vipaji na uwezo wa wachezaji kucheza nafasi mbalimbali lakini bila kuua mfumo wa kujilinda na kushambulia.
Lwandamina kikosi cha kwanza amekiingiza uwanjani kwa mfumo wa 3-5-1-1( 3-5-2). Nyuma wakisimama Kelvin Yondani , Andrew Vicent na Justin Zullu. Juma Abdul , Haji Mwinyi , Thabani Kamusoko , Saimoni Msuva na Emanuel Martin wakimaliza kati na juu wakisimama Haruna Niyonzima na Juma Mahadhi.
Lwandamina baada ya kuona mechi mbili tatu za timu za Zanzibar , amegundua uwezo wao mkubwa kuchezea mpira ( holding ) hususani eneo la kiungo na kushambulia kwa kutumia wings. Zimamoto waliwapa tabu sana Azam FC mechi ya kwanza kutokea kati na kwenye wings , hii imemfanya George Lwandamina kujaza viungo ili kujihakikishia kumiliki mpira na kuwakataa Zimamoto kuitawala timu yake kati na kwenye wings.
Juma Mahadhi ambaye mara nyingi hucheza kama winga leo kampanga kama mshambuliaji wa kati lakini kimbinu false 9 akicheza kwa kurudi chini eneo la kiungo ili kuivuta beki ya Zimamoto kuondoka kwenye muhimili wao na hili lilimsaidia Msuva kupata nafasi ya kuchomoka muda mwingi baada ya hii tactical screening. Utaona Juma Mahadhi hakufanya attempt yoyote kama main striker lakini alikuwa akifanya holding kuwagawa walinzi wa Zimamoto.
Kama Zimamoto wangejua mbinu za Lwandamina leo zilimzunguka Justin Zullu ambaye huyu ndie alikuwa anaamua Yanga wacheze vipi , basi huenda wangetoka na kitu.
Licha ya timu kucheza bila mipango sahihi iliyonyooka kwa kujenga muunganiko sahihi kimbinu toka nyuma hadi mbele lakini Zullu ndie aliyekuwa akianzisha mashambulizi yote au kutanua dimba na kuwaruhusu wenzake wauchezee mpira ( holding/give and go passes) . Alicheza chini kama kiungo mkabaji lakini akijenga kombinesheni na Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima ambaye leo alipangwa kama kiungo mshambuliaji " huru "
Utagundua Lwandamina ameanza kuijenga Yanga katika mbinu zile zile za Zesco United. Outfielder players wote kuwa na uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani kama viraka ( versatility) . Timu inashambulia yote na kukaba yote .
Mfumo huu unawezekana endapo mwalimu atawafanyia rotation wachezaji kucheza nafasi mbalimbali lakini bila kuathiri mfumo wa timu nzima kiulinzi na kushambulia ( chemistry/ tempo and rythm ) . Hii utafanikiwa ukiwa na key players kulinda mfumo wako na ndio maana leo Justin Zullu hakutolewa uwanjani leo akisimamia kazi hii.
Hii pia imejionesha kwa kumtoa Mahadhi na kumwingiza Oscar Joshua kucheza tisa ingawa yeye ni beki wa kushoto huku Kaseke baada ya kuingia akijaribu kucheza na Zullu kati kama " double six .


Post a Comment