Kocha msaidizi wa Yanga SC Juma Mwambusi amesema kuelekea mchezo wao wa kwanza katika michuano ya klabu bingwa Afrika, wamejiandaa vizuri kuwavaa wapinzani wao ugenini katika visiwa vya Comoro.
" hatujawahi kuiona Ngaya ila tunaiheshimu kama timu nzuri baada ya kupata taarifa zao. Wanawachezaji wawili toka Ivory Coast na namba kubwa ya wachezaji wao wa ndani wana maumbo makubwa na wazuri kucheza mchezo wa nguvu na kasi muda wote. Hivyo tunajipanga kupambana nao "
Mwambusi akihojiwa na kurugenzi ya habari ya Yanga SC alikwenda mbali zaidi kwa kusema ; Ngaya wana vikombe vinne hivyo si timu ya kubeza na wanafahamu wataleta upinzani mkali kutaka alama tatu kwao lakini wao wamejipanga katika hilo.
Mwambusi akitoa hali ya kambi yao , amesema katika mchezo wao na Ngaya watawakosa washambuliaji wao wawili kwa matatizo ya kiafya. Donald Ngoma ameumia eneo la kiuno na atakaa nje kwa wiki mbili akiendelea na matibabu na Malimi Busungu ametoka kulazwa hospitali kwa baada ya kuumwa malaria kali hivyo wawili hao wataukosa mchezo wa jumapili visiwani Comoro.
" ukiondoa wawili hao kikosi kipo katika hali nzuri kimchezo na kisaikolojia. Kwa kudra za Mungu na maombi ya watanzania tuna imani kushinda mchezo huo ugenini"


Post a Comment