Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: VICENTE BOSSOU AUNGURUMA USHIRIKI WA TOGO AFCON
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Godlisten Anderson Chicharito Mtandao wa Balozi Blogsport umefanya mahojiano na mlinzi wa kati wa Yanga SC Vicent Bossou baada ya kuwasi...

Na Godlisten Anderson Chicharito

Mtandao wa Balozi Blogsport umefanya mahojiano na mlinzi wa kati wa Yanga SC Vicent Bossou baada ya kuwasili nchini akitoka kuitumikia timu yake ya Taifa ya Togo katika michuano ya AFCON nchini Gabon.

Katika mahojiano hayo , Vicent Bossou amezungumzia ushiriki mzima wa timu hiyo katika michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika.

Bossou anaanza kwa kusema " timu yetu ni nzuri sana kwa uwezo mmoja mmoja wa mchezaji ukiangalia namba kubwa ya wachezaji wanacheza ligi kubwa na bora duniani lakini kilichotufanya kuondolewa hatua ya makundi ni mwalimu Roy kushindwa kuleta umoja ndani ya timu. Wachezaji wakubwa walikuwa wakiamua wanavyotaka wao na kukinzana na mwalimu mara kwa mara. "

Togo inayoundwa na wachezaji kama viungo Alaixys Romao (Olympiacos, Greece), Matthieu Dossevi (Standard Liège, Belgium), Floyd Ayité (Fulham, England), Henritsè Eninful (Doxa Katokopias, Cyprus), Lalawele Atakora (Helsingborgs, Sweden), Prince Segbefia (Goztepe, Turkey), Ihlas Bebou (Fortuna Dusseldorf, Germany), Franco Atchou (Dyto), Serge Gakpe (Genoa, Italy) utaona namba yao kubwa wanacheza soka la kulipwa barani ulaya ndio wanaolalamikiwa na Bossou kushindwa kumuheshimu mwalimu na kuvunja umoja kitimu hali iliyowafanya kuishia hatua ya makundi.

Nje na sababu hiyo Bossuo alikwenda mbali zaidi na kusema mwalimu Roy ilifika wakati wachezaji hawakutaka kufuata mfumo wake na kujiamulia wanavyotaka wao.

" mechi yetu ya kwanza na  Ivory Coast ambayo tulitoka sare ya 0-0 kama wachezaji wangekuwa kitu kimoja basi tungeshinda. Timu ilikosa kiongozi ndani ya timu wa kuwashawishi wenzie wamsikilize mwalimu . Adebayor wengi walikuwa wakimdharau au kumuona hana sauti ndani ya timu hiyo kutokana na yeye kutokuwa na timu. "

Vicent Bossou amegusia pia uchache wa watazamaji kwenye michuano hiyo ukisababishwa na vurugu za kisiasa.

" ni ngumu kuona watu wengi kama hapa nchini wakicheza Yanga na Simba kutokana na hofu ya usalama wao na wakati mwingine wana usalama walikuwa wanaruhusu namba ndogo ya watazamaji ambao wanaweza kuwamudu."

Bossou analia na umoja ndani ya timu yake kama silaha ya mafanikio kwa nchi hiyo kisoka.  " mathalani Drogba alikuwa akisikilizwa ndani ya Ivory Coast enzi akiichezea timu yake ya taifa ndivyo ambayo tunapaswa kuiga kama tunataka mafanikio. Angalia umoja waliokuwa nao Cameroon licha ya wachezaji wao wakubwa kugoma kuichezea timu yao lakini waliokuwepo walijua thamani ya taifa lao na kujituma zaidi na wakabeba kombe"

Vicent Bossou amerudi nchini kuitumikia klabu yake ya Yanga baada ya kumalizika michuano hiyo na mapumziko mafupi ya ndoa yake . Bossou amejipanga kujifua zaidi ili mwalimu Lwandamina amtizame kwenye kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa awali.

Togo waliondolewa katika michuano ya AFCON hatua ya makundi baada ya kwenda sare ya 0-0 na Ivory Coast , kupigwa 3-1 na Morroco na kutandikwa tena 3-1 na Congo DRC.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top