Ikiwa ni wiki mbili tangu timu ya taifa Zimbabwe (The Warriors) itolewe kwenye michuano ya mataifa ya Afrika AFCON nchini Gabon katika hatua ya makundi, Chama cha soka cha ZIMBABWE (ZIFA)kimemfukuza kazi aliyekua kocha wa kikosi hicho mzimbabwe Kalisto Pasuwa.
Kwenye michuano ya AFCON Zimbabwe ilifanikiwa kupata pointi moja katika michezo mitatu iliyocheza na kushika mkia katika Kundi B, ambapo ilitoka sare na Algeria 2-2, ilifungwa 2-0 na Senegal, na ya mwisho ilichezea kwa kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa Tunisia.
Baada ya kutoridhishwa, ZIFA imeamua kumpiga chini Pasua baada ya matokeo mabaya, bado awajatangaza ni nani atakuwa mrithi wake.
Hapo awali Kalisto Pasua aliingoza Zimbabwe kufuzu AFCON baada ya miaka 10, kwani mara ya mwisho walishiriki michuano ya mwaka 2006 iliyofanyika nchini Misri na kushuhudia Zimbabwe pia ikimaliza ya mwisho katika Kundi D baada ya kuambuliwa pointi 3.
Post a Comment