na Samuel Samuel
Huyu ndio mchezaji wa kwanza katika historia ya soka la kulipwa la Uingereza kupiga penati.
Mapigo ya mikwaju ya penati katika soka historia yake inaanzia mwanzoni mwa miaka ya 50 baada ya mataifa kama Yugoslavia , Sweeden , Bulgaria katika ligi zao za ndani kuachana na mtindo wa kuamua mechi kwa sarafu baada ya matokeo ya sare.
Kwa mara ya kwanza nchini Yugoslavia katika ligi yao ya Yugoslav Cup mwaka 1952 walitumia njia ya kuamua matokeo ya mechi kwa penati na kuachana na mtindo wa kurusha juu sarafu. Coppa Italia nao walitumia mfumo huu mwaka 1958-59.
Rasmi urasimishwaji wa mapigo haya ya penati katika mfumo huu wa kisasa uliratibiwa na shirikisho la soka duniani FIFA mwaka 1970 baada ya barua maalumu kutoka kwa mdau mkubwa soka kipindi hicho toka Israel , Yosef Dagan. IFAB ( International Football Association Board ) waliipotia barua yake na wao kufanya marekebisho yao vizuri na kuingiza rasmi mfumo huu katika kanuni na sheria za FIFA .
George Best winger wa Manchester United ndio mchezaji wa kwanza katika soka la kulipwa kupiga penati katika mechi ya kombe la Watney ngazi ya nusu fainali dhidi ya Hull City mwaka 1970. Mechi ilipigwa katika jiji la Hull.
Best alikwamisha mkwaju huo nyavuni na kujiandikia historia hiyo huku Denis Law akiweka pia rekodi yakuwa mchezaji wa kwanza kukosa penati. Manchester United walifuzu kwenda fainali kwa ushindi wa 4-2.
Ngazi ya kimataifa zilianza rasmi kutumika mwaka 1971 katika fainali ya UEFA European Cup.
Katika michuano ya kombe la dunia, ilipitishwa rasmi mwaka 1978 ingawa haikutumika mpaka michuano ya mwaka 1982 lakini katika historia ya kombe la dunia , fainali za mwaka 1994 nchini Marekani ndio za kwanza kumtoa bingwa kwa mikwaju ya penati baada ya Brazil kumpiga Italy kwa penati 3-2 na mwaka 2006 baada ya Italia kumpiga Ufaransa 5-3.


Post a Comment