Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: HUYU NDIO MCHEZAJI WA KWANZA KUFUNGA GOLI KOMBE LA DUNIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
na Samuel Samuel Ni miaka 87 sasa imetimia toka kuanzishwa kwa michuano ya kombe la dunia na muhasisi wake Jules Remit raisi wa tatu wa FI...


na Samuel Samuel

Ni miaka 87 sasa imetimia toka kuanzishwa kwa michuano ya kombe la dunia na muhasisi wake Jules Remit raisi wa tatu wa FIFA ambaye ana rekodi ya kipekee kwa kukaa madarakani kwa miaka 33!.

Michuano hii ambayo kabla ya mwaka 1974 ilijulikana kama Jules Remit ( JULES REMIT TROPHY) kabla ya kubadilishwa na kuchukua jina la sasa FIFA WORLD CUP , ina historia nyingi za kuvutia na kushangaza sana .

Ni michuano ambayo imejizolea umaarufu mkubwa duniani toka kuhasisiwa kwake na kuingia katika mizazi ya matukio muhimu yenye mvuto wa kipekee duniani . Inasadikika fainali za kombe la dunia katika mchezo huu wa soka ndio tukio lenye kuongoza kuvuta hisia za watu wengi zaidi duniani likifuatiwa na uchaguzi wa maraisi wa Marekani.

Lucien Laurent si jina geni kwa wale wadau vindakindaki wa mchezo wa soka . Ni jina ambalo lina uzito wake wa kipekee katika historia ya soka na michuano ya kombe la dunia kwa ujumla wake.

Huyu ni marehemu kwa sasa; ni mmoja kati ya magwiji ya soka duniani waliyoibuka mwanzoni mwa karne ya 20 wakiathirika vibaya na machafuko ya vita ya pili ya dunia iliyoanza mwaka 1939 na kumalizika mwaka 1945. Vipaji vingi vya soka vilipotea baada ya mchezo wa soka kusimama mwaka 1938 Italia akiwa bingwa wa dunia kupisha kisu cha vita kumwaga damu duniani.

Lucien alikuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa ambaye ndie anashirikia rekodi yakuwa mwanadamu wa kwanza kutikisa nyavu katika michuano ya kombe la dunia.

Lucien akicheza kama inside right kunako dakika ya 19 ya mchezo aliwainua wafaransa vitini kwa goli zuri baada ya kuachia kombora katikati ya walinzi wa Mexico. Hilo ndio goli la kwanza kufungwa katika historia ya kombe la dunia. Hiyo ilikuwa mwaka 1930 katika mchezo uliowakutanisha Ufaransa na Mexico ambapo Ufaransa waliibuka na ushindi wa goli 4-1.

Magoli mengine ya Ufaransa yalifungwa na Andre Maschnoti aliyefunga magoli mawili na Marcel Langiler aliyehitimisha karamu hiyo. Goli la kufutia machozi la Mexico lilitiwa kambani na mlinzi wa kulia Juan Carreno.

Laurent Lucien alizaliwa mwaka 1907 katika jimbo la Saint-Mauredes-Fosses na alifia Besancon akiwa na umri wa miaka 97 mwaka 2005, mwezi Aprili tarehe 11.

Alipata kuichezea timu yake ya Ufaransa toka mwaka 1930 mpaka mwaka 1936 akicheza mechi 23 na kufunga magoli 14. Ni mmoja kati ya watu waliokuwa wakipewa heshima ya kipekee na Shirikisho la soka duniani kabla ya umauti wake .

Fainali za kombe la dunia mwaka 1998 taifa lake la Ufaransa likibeba kombe hilo dhidi ya Brazil, alitoa mwaliko wa kipekee wa timu hiyo kumtembelea nyumbani kwake na alikuwa akimuhusudu sana aliyekuwa kiungo mshambuliaji w timu hiyo Zinedine Zidane 'Zizzou'. 

Timu ambayo alipata kuichezea kwa muda mrefu sana ni CA Paris . Kwa mara ya kwanza aliichezea kuanzia mwaka 1921 mpaka mwaka 1930 . Baada ya michuano ya kombe la dunia alitimkia FC souchax Montbellard aliyoichezea kwa miaka miwili tu mpaka mwaka 1932. CA Paris baada ya kuyumba sana kwenye safu yao ya ushambuliaji mwaka 1931 , 1933 walimrudisha tena Lucien Laurent awasaidie kuwanusuru wasishuke daraja ambapo baada ya msimu kwisha alitimka tena. Ni mchezaji ambaye alikuwa anatakiwa na vilabu vingi kipindi hicho hali iliyomfanya kutokudumu katika timu moja kwa muda mrefu.

Alistaafu soka rasmi mwaka 1946 akiwa na klabu ya mtaani kwake Bensacon RC mji aliofia . Vurugu za vita pia zilichangia yeye kuachana na soka.

Gwiji huyu ana historia ya uchungu sana na vita vya pili vya dunia . Mwaka 1939 vita ilipoanza alilazimishwa kwenda vitani na nchi yake . Vijana wengi wakati huo walipewa mafunzo ya muda mfupi na kuingia vitani kwa huyari au lazima.

Akiwa vitani mwaka 1940, patuni yao ilitekwa na majeshi ya Ujerumani . Wengi walikufa na kuumizwa vibaya lakini mshambuliaji huyu umaarufu wake wa soka katika michuano ya kombe la dunia mwaka 1930 ulimsaidia kwa askari wa Kijerumani kuona fahari kumweka kama mateka wa kivita ( prisoner of war ) . Alikaa mateka kwa miaka mitatu akifanya kazi ngumu katika vikosi vya Nazi na kutoa burudani ya kupiga danadana au kuonesha uwezo wake kumiliki mpira ( controlling ) mbele ya maafisa wa jeshi la Ujerumani.

Kutekwa kwa Lacien lilikuwa pigo kw Ufaransa kutokana na umaarufu wake na vitendo vya fedheha ambavyo Wajerumani walikuwa wakimfanyia kama dhihaka kwa wafaransa.

Nidhamu , ucheshi , kipaji chake viliwafanya wajerumani mwaka 1943 kumwachia huru wakati ambao nao pia vita ilianza kuwashinda.

Kipindi chote cha uhai wake Lucien alikuwa akitoa rai zake duniani kwa mataifa makubwa kusimamia amani ya dunia akitaka vijana wengi yasiwakute yaliyompata yeye vitani kipindi hicho.

Baada ya kuachana na soka alikuwa kocha wa vijana wadogo pia aliweka historia ya mchezaji pekee aliyebaki hai kushuhudia fainali za kombe la dunia nchini kwao mwaka 1998 katika kikosi cha Ufaransa kilichocheza fainali za mwaka 1930. Wenzake wote walikuwa tayari wametangulia mbele za haki.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top