Simba na Vunjabei ni business partners. Msingi wa mkataba wao sio matangazo kwenye jezi ya Simba au "visibility". Msingi wa mkataba wao ni biashara ya jezi.
Mo Dewji ndiye ambaye msingi wa biashara yake na Simba ni visibility.
Yanga na GSM ni business partners. Msingi wa mkataba wao ni biashara ya jezi sio visibility kwenye jezi ya Yanga.
Lakini Msingi wa mkataba wa TFF na GSM ni visibility. Hapa sasa GSM anataka kupata visibility kwenye timu zote za ligi kuu.
Kwa sababu msingi wa mikataba hiyo iko tofauti hakuna conflict of interest wala unfair competition. Simba wana hoja dhaifu sana. Kwenye andiko Lao naona Kiingereza tu ndio kingi kuliko hoja.
Anyway maandishi ya Kiingereza yakitumika kuandika hoja hata kama hoja ni dhaifu unaweza kudhani ni hoja ya maana😃😃😃
Kimsingi anayelalamika hapo sio Simba bali ni Mo Dewji ambaye msingi wa biashara yake na Simba ni visibility.
Mo Dewji kwa sababu zake za kibiashara hataki GSM wapate mileage. Dawa ni rahisi sana. Atoe mzigo TFF.
TFF hawawezi kutekeleza interest za klabu zote. Ziko nyingi mno. Kila mmoja akitoa masharti mdhamini huyu hatumtaki mwishowe TFF watakosa mdhamini.
Klabu ndio zinatakiwa zifuate masharti ya TFF. Uamuzi ni wao TFF. Waamue kufyata mkia au wakomae. Mpaka sasa TFF wako kwenye mstari. Wakiendekeza Simba mpira utakosa wadhamini.
Katika hili wanaoathirika ni wengi. Wanaoathirika ni timu zote za ligi kuu. Unaoathirika ni mpira wa Tanzania. Mpira wa nchi hii ni mkubwa kuliko Simba. TFF tumianeni mamlaka yenu.
Yote fanyeni lakini mhakikishe hawa jamaa wanakuja uwanjani Desemba 11. Tunawasubiri kwa hamu.
Post a Comment