N
imepata bahati ya kupitia malalamiko ya klabu ya Simba sc juu ya udhamini baina ya GSM,Bodi ya ligi na TFF na kuna hoja wamezitoa hivyo nami nitajielekeza kwenye hoja zao kama ifuatavyo
1.CEO wa klabu ya simba sc amenukuliwa akisema kuwa mkataba baina ya GSM,Bodi ya ligi na TFF wao kama simba sc hawakushirikishwa,Sasa sijui amesahau Madam CEO kwani Mkataba baina ya NBC,AZAM media,TBC na Bodi ya ligi na TFF walishirikishwa wakati wa mchakato?Jibu ni hapana sasa iweje leo mkataba mmoja tu wa GSM ndio walete nogwa za kitoto?
2.Hivi madam CEO na watu wake wa Simba ina maana hawajui kuwa mwenye ligi ni Bodi ya ligi na TFF? kama ndivyo wao kimtakabata kama vilabu vingine kwa maana ya wadau wanatakiwa kupewa wajibu na maelekezo ya kutii mikataba yote itakayosainiwa na shirikish.Niwarudishe nyuma mnakumbuka kuna wakati vilabu vya Simba na Yanga vililalamika juu ya udhamini wa Azam media na TFF juu ya kwanini wapewe pesa sawa na vilabu vingine,hapa unagundua kuwa mchakato wa kutafuta na kupata udhamini ni swala la bodi ya ligi na shirikisho la soka.
3.Wadau kama vilabu wao ni kama walaji ambao wanapatiwa majukumu na wajibu wao juu ya mikataba mbalimbali inayosainiwa baina shirikisho na wadhamini mbalimbali.
4.Pia Bidada CEO ameibua hoja ya kuwa wakati mkataba unasainiwa wao kama klabu hawakuwa sehemu ya waalikwa,ni jambo la kushangaza ikiwa CEO wa timu inayojihita timu kubwa kushindwa kujua taratibu za kawaida kama hizi,labda nimkumbushe msimu uliopita siku ambayo Bodi ya ligi na TFF ilivyokuwa inasain mkataba na Azam media klabu ya Yanga haikuwa na mwakilishi yeyote kwani siku inafanyika hafla ya kusaini Yanga walikuwa na mchezo na Mwadui wa kombe la Asfc ila mambo yaliendelea,lakini pia ni uamuzi wa bodi ya ligi kualika vilabu na sio lazima au sehemu ya makubaliano ya kimkataba kuwa siku ya kusaini basi timu zote ziwepo,hivyo bidada CEO kwakuwa amevamia kwenye soka inapaswa apewe shule na wenzake na sio kukurupuka mkataba ni mali ya Bodi ya ligi,TFF na mdhamini.
5.Bidada CEO hakuishia hapo akaja na ishu ya Conflict of interest kuwa kwanini GSM anaidhamini Yanga pia anadhamini Ligi na kuhisi Yanga sc watanufaika ikizingatiwa Yanga imekosa ubingwa misimu minne,inasikitisha sana ila ngoja tumpe shule na kumkumbusha kuwa msimu uliopita Vodacom ndio walikuwa wadhamini wa ligi na pia walikuwa wadhamini wa klabu ya Namungo sasa swali vipi Namungo walibeba ubingwa?au hoja ni kwakua Yanga sc? Madam ukiwa na kikosi imara,bora na mazingira mazuri ubingwa utapatikana kuanza sasa kuogopa na kutaka kuwafumbaza washabiki wenu ni uhuni usio kubalika chezeni mpira na uzuri mnasema nyie mmepiga hatua sasa tuone ukubwa wenu uwanjani acheni hizi chuplichupli.
6.Lakini pia nani asiyejua kuwa mdhamini wa kombe la shirikisho ni Azam media kwa misimu kadhaa sasa,Je toka azam imeanza kudhamini wamechukua ubingwa huo mara ngapi? Iweje hofu iwe kwa GSM na yanga?Akaibuka mchumia tumbo mmoja akaja na hoja kuwa viongozi wa Azam media wao sio viongozi wa Azam fc hivyo mkataba upo salama sasa niwakumbushe kitu Patrick kahemele ni kiongozi wa Azam media je hakuwahi kuwa katibu mkuu wa Simba sc? Je nasisi tuseme Simba sc wananufaika na udhamini wa Azam media kupitia Uwepo wa Mr.Patrick? Bidada umesomea wapi mwenzetu?
7.Wakaibua hoja nyingine dhaifu sana kuwa iweje GSM awavalishe Yanga sc pia nembo yake iwe kwenye timu zingine mfano jezi ya simba itakuwa na GSM na vunja bei sasa wanasahau kuwa GSM ni mkusanyiko wa makampuni mengi yanayotoa huduma tofauti na kila kampuni itaka kujitanua na kufanya biashara na wateja wengi hivyo GSM foam anaweza kudhamini NBC preamiar league Huku Kampuni nyingine ya GSM ikadhamini ligi ya wanawake,huku kampuni nyingine ya GSM ikadhamini Ligi daraja la kwanza kwani makampuni yanayofanya kazi tofauti,ni kama Mdhamini wao Mo alivyo na makampuni lukuki,MO pikipiki,Mo nazi,Mo masufuria,Mo bajaji,Mo vikoba na mengine mengi.
Watanzania tumelilia muda mrefu uwepo wa wawekezaji na wadhamini katika soka letu ili Taifa lipate pesa lakini pia vijana wapate ajira sasa TFF inapojitahidi kuweka mazingira rafiki kwa vilabu alafu inatokea timu moja ya watu wabinafsi na wasio jielewa na kuleta hoja dhaifu haikubaliki.
Post a Comment