Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: SIMBA WANAPASWA KUTOFAUTISHA GSM NA YANGA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kwa siku kadhaa Sasa kumekuwa na mjadala mzito sana kwa watu wa mpira hapa nchini na kubwa zaidi Ni pale watu wanapohoji kwa kutumia ushabik...



Kwa siku kadhaa Sasa kumekuwa na mjadala mzito sana kwa watu wa mpira hapa nchini na kubwa zaidi Ni pale watu wanapohoji kwa kutumia ushabiki ndani yake.

Simba wanalalamika kwanini wavae nembo ya mdhamini mwenza (GSM) ilihali hakuna sheria inawataka wafanye hivyo.

Ngaja niwaambie Simba kanuni na sheria Ni pana sana ndugu zangu kama mnatekeleza basi mnapaswa kutekeleza kwa upana huo huo. Ni kweli sheria inasema mdhamini mkuu ndiye anapaswa kukaa bega la kulia lakini ukisoma kanuni zingine za chini kuna kipengele kinasema, timu zinapaswa kuvaa nembo za wadhamini kama kutakuwa na maelezo maalumu, je! Simba hawajapewa maelezo maalumu? 

Mpira wa Sasa unahitaji pesa ili timu ziweze kupata mahitaji yake kwa wakati, kwahio hakuna sababu ya kuwazuia wadhamini kuja kuwekeza pesa.

Simba wanahoja dhaifu sana ambazo hazikupaswa kutolewa na watu kama wao. Kanuni zipo wazi wanapaswa kuzisoma kwa ujumla wake na sio kipengele kimojakimoja.

Wadhamini wanapaswa kuungwa mkono kwa asilimia 100 ili mpira wetu uweze kufika mbali na haijalishi ni Nani anakuja kudhamini.

Kinachowapa wasi wasi Simba Ni mahusiano ya Yanga na GSM, kitu ambacho kiko wazi hizi Ni taasisi tofauti kabisa na haziingiliani. GSM Ni mdhamini wa Yanga na sio mmiliki wa Yanga hivyo haina athari yeyote kwenye maendeleo ya soka letu.

Rudi nyuma kidogo Vodacom walidhamini ligi lakini pia walidhamini Namungo na hakukuwa na unfair yoyote ile Leo hii kwanini kisa Yanga? Au Azam media si ndio mdhamini wa kombe la ASFC je Azam wamewahi kupendelewa? 

Simba wanapaswa kutafakari kwa kina zaidi ili wasizuie klabu zingine kupata pesa kutoka kwa wadhamini.

Na @ramanzwalla

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top