Wakati fulani hayati Bob Marley alipata kufanya mahojiano na kituo cha Radio nchini Jamaica kuhoji maisha yake binafsi na familia yake .
Aliulizwa kwanini mbali na umaarufu wake na utajiri, familia yake inaishi maisha ya kawaida sana kama zilivyo familia nyingi pale Kingston Jamaica.
Bob alijibu kwa ufupi sana, “ utajiri wa mwanadamu ni uhai wake na akili ya kutambua thamani ya vile vinavyomzunguka. Utambuzi huo, huja kwa kutambua binafsi kutokana na IQ yako au kufundishwa na wenye maono juu ya hilo” - Marley
Kwa miaka mingi klabu za Simba na Yanga zimeendeshwa kwa mifuko ya wafadhili na wahisani huku wanachama wao wakiwa watu wa kupiga makofi tu au kuwa sehemu ya kuchota kile ambacho wafadhili na wahisani wanakiweka kwa ajili ya klabu au timu.
Hapo ndipo tulipozalisha mafisadi wa timu, chawa na makomandoo ambao waligeuka kupe pasi kuweka jasho lao kwa vilabu hivyo.
Mfumo huu wa wanachama kuchangia vilabu vyao kupitia cards kwa Yanga na miamala mbalimbali kwa Simba kwa program ya ujenzi ya uwanja, ni njia sahihi ya kuwajenga wanachama kutambua thamani na umaana wa vilabu vyao na mali zao . Hicho ndicho Marley alikijenga kwa familia yake kiasi kwamba mpaka leo watoto wake na familia kwa ujimla hawajaharibu FAME yake.
Si kwamba vilabu hivi vitategemea tu michango ya wanachama wao, bali ni nyenzo muhimu sana katika kuwapa utashi wa kutambua uchungu na raha ya umiliki wa vilabu vyao.
Samuel Samuel
Post a Comment