Kazi ya kampuni ya K NET itakuwa ni kutengeneza kanzidata za mwanachama ambazo zitapelekwa kampuni ya N CARD(TTCL) kwa ajili ya kutengeneza kadi ya mwanachama.
Ufafanuzi wa namna ya kupata kadi ni kama ifuatavyo:-
✓• Unalipia Tsh 2,000/= ya fomu (kama tayari wengi tulivyofanya kwenye tawi letu) halafu utajaziwa taarifa zako kwenye fomu yako (ambazo tayari tunazo).
✓• Baada ya kujaziwa hizo taarifa utatakiwa kulipia TZS 29,000/= ambazo ni kwa ajili ya;
• *A*- TSh 5,000/= kulipia kadi na
• *B* - Tsh 24,000/= ada ya mwaka jumla ndio 29,000/=
✓• Hizi TZS 29,000/= hutalipa/hutalipia tawini kama ulivyo lipa TZS 2,000/= za fomu, bali utalipia kupitia simu yako hivyo zitaingia moja kwa moja Makao Makuu kwenye akaunti ya Yanga SC.
✓• Pindi utakapolipia hizo Tsh 29,000/= taarifa zako kupitia kwenye fomu uliyojaza zitapelekwa Makao Makuu ya Yanga SC nawe utapata ujumbe mfupi kwenye simu
yako kuwa fedha na taarifa zako tayari zimepokelewa.
✓• Taarifa zako sasa zitaingizwa rasmi kwenye mfumo wa utengenezaji kadi kupitia makampuni niliyoeleza hapo awali ndipo kadi yako ikishakuwa tayari utapokea tena ujumbe mfupi kwenye simu yako ukijulishwa kuwa kadi yako ipo tayari na utapewa utaratibu wa namna itakavyokufikia.
✓• Nimeona nitoe ufafanuzi huo ili kama kuna mtu alikuwa haelewi kinachoendelea apate angalau pa kuanzia.
Asante!
Post a Comment