Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: YANICK BANGALA LITOMBO ‘ the machine ‘
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Umoja wa mashabiki wa AS Vita mwezi July mwaka jana 2021, walihitisha kikao cha ghafla na viongozi kuhoji kwanini Yanick Bangala Litombo ana...


Umoja wa mashabiki wa AS Vita mwezi July mwaka jana 2021, walihitisha kikao cha ghafla na viongozi kuhoji kwanini Yanick Bangala Litombo anaondoka?! Uongozi wao ulikuwa na jibu jepesi sana ambalo lilitolewa katika mazingira ya uchungu sana . “ tumejitahidi sana kumpa ofa mpya lakini amesisitiza kuondoka “

Baleke Byemba mmoja wa mashabiki wakubwa wa AS vita pale Kinshasa, aliandika kwa uchungu sana katika ukurasa wake wa Facebook, akisema “ Bangala ni kama umechomoa injini kwenye gari letu daah “

Machozi ya Baleke ukiyatafakari sana utayaelewa sasa kwa kazi ambayo Litombo anaifanya pale Yanga SC . Huyu ndio silaha namba moja ya Nabi Nasreddine katika patterns zake zote za kushambulia na kujilinda . 

Bangala anakufanya uuone ubora wa Diarra pale langoni akisimamia vyema mfumo mzima wa timu kujilinda aidha acheze kama mlinzi au kiungo mkabaji. 

Aucho ni doctor haswa wa mpira eneo la kati , lakini ukitaka vipimo vyake vya kitabibu viwe sawa, akicheza double pivot na huyu mwamba na umoja huo automatically unaifanya safu ya ushambuliaji kuwa ya moto zaidi.

Bangala ni stereo type ya wachezaji viraka uwanjani ambao wana akili kubwa ya mpira , nguvu na maarifa ya kusimamia umbo la timu liwe imara muda wote . 

Natamatisha kwa kusema huyu kwangu ndio mchezaji ambaye anasimama kama nyota wa kigeni ambaye ametimiza majukumu yake uwanjani kwa zaidi ya asilimia 80 kwa nusu ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara.

Samuel Samuel 
@ 2022

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top