1. Mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu baada ya mabadiliko ya katiba yetu ambayo imesajiliwa katika ofisi ya msajili wa vilabu vya michezo.
2. Wanachama wote wa yanga watahakikiwa kwa kutumia fomu maalum itakayojazwa na mwanachama na kusainiwa na viongozi wa kila tawi. Hakuna mwanachama atakayesajiliwa kupitia Makao Makuu ya klabu.
3. Mwanachama atalipia 29,000/= kwa ajili ya kupata kadi ya uanachama.
4. Wanachama wote watasajiliwa kwa njia ya dijitali. Hii itamsaidia mwanachama kupata taarifa zake kupitia simu yake ya kiganjani.
5. Kila tawi litanunua kitabu chenye kurasa 100 na katiba moja kwa kiasi cha shT 40,000/=. Kila tawi likiishanunua hizo nyaraka litapatiwa hati ya utambulisho kuwa ni tawi rasmi.
6. Kutakuwa na usajili wa mashabiki wa klabu.
7. Hadi sasa tunayo matawi 167 ambayo yamesajiliwa klabuni.
UWAKILISHI WAKATI WA KUWACHAGUA VIONGOZI WA KLABU
1. Kila tawi litakuwa na wajumbe 5 ambao watashiriki mikutano mikuu yote ya klabu.
2. Uchaguzi wa kila tawi, utawachagua vingozi 8 ambao ni:
. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, katibu, katibu msaidizi, mweka hazina na wajumbe watatu tu.
Kwa muhtasari hayo ndiyo ya msingi. Mengi yako kwenye fomu za kuhakiki na katiba yetu mpya.
Florian Mbeo
MSHIRIKI WA MKUTANO
Post a Comment