Michuano ya AFCON ya msimu huu yamewapa sana fursa wachezaji wengi wenye umri mdogo katika nchi tofauti ambao wataonyesha vipaji vyao kwenye michuano hiyo ya AFCON
Kuna wachezaji 4 wenye umri mdogo wa kuanzia miaka 17 mpaka 20 walioitwa kwenye vikosi vya timu za taifa za Sierra Leone,Mauritania,Ghana na Tunisia.
1.BEYATT LEKWEIRY (MAURITANIA ) - 16years 8months
Kiungo wa Mauritania ndiyo mchezaji mdogo zaidi kwenye michuano hii ya AFCON 2021
Kocha mkuu wa Mauritania Didier Gomes Da Rosa alimuita mapema kwenye kikosi chake kitakachoshiriki AFCON.
2.IBRAHIM SESSAY (SIËRRA LEONE) - 17years 2months
Golikipa huyu wa Sierra Leone ameitwa kwenye kikosi akiwa ni mchezaji wa 2 mwenye umri mdogo kwenye michuano ya AFCON
3.ABDUL FATAWU ISSAHAKU (GHANA) 17 years 10 Months
Kiungo mshambuliaji huyu wa Ghana anayeitumikia klabu ya Dreams FC kwa mkopo akitokea Steadfast FC ya Ghana amejumuishwa kwenye kikosi cha Afcon baada ya kuonekana anafanya vizuri
Aliwahi kucheza timu ya vijana Ghana u17 na U20 kwa mafanikio makubwa.
4.HANNIBAL MEJBRI (TUNISIA) 18years 11 months
Kiungo wa Manchester United ya Vijana amejumuhishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tunisia kitakachocheza michezo ya AFCON nchini Cameroon.
Kinda gani wa kwetu anatakiwa aanze kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa.
Tepse Kinda ^Fundi kutokea Azam FC
ReplyDelete