Kocha Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi ambacho kitaingia kambini Alhamisi tayari kuanza kujiwinda kwa ajili ya Malawi.
Stars itashuka dimbani Oktoba 9 kuivaa Malawi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi yake ya kwanza kuwania kucheza Kombe la Dunia.
Kikosi kimetangazwa leo na Kocha Msaidizi, Hemed Morocco.
Makipa:
Ally Mustapha, Aishi Manula na Said Mohammed.
Mabeki:
Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mohammed Hussein, Hassan Isihaka, Juma Abdul, Shomary Kapombe na Mwinyi Haji.
Viungo:
Himid Mao, Said Ndemla, Salum Telela, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Simon Msuva na Deus Kaseke
Washambuliaji:
Rashid Mandawa, John Bocco, Mrisho Ngassa, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Farid Mussa.


Post a Comment