1. Ali Mustafa Batezi.
Nadhani sasa amekomaa na falsafa za mechi ya watani wa jadi. Jana alionesha utulivu mkubwa sana na alizijua vyema mbinu za kupoza tension ya game pale timu ama backline ilipokuwa inakosa utulivu. Mambo hayo yalimpa sana umaarufu Juma Kaseja akiwa Simba SC. Kuna wakati mwanzoni mwa mchezo Nadir na Yondani walianza kuingiliana kwenye marking lakini Mustafa alizungumza na team Captain na hali kutulia. Tatizo la kuchelewa kutoka na kucheza krosi limepungua sana . Hongera Pondamali. Dakika ya 58 alifanya clearance nzuri nje ya 18 baada ya Mwinyi kuzidiwa maarifa na Kazimoto. That was good and sensed maturity. Nakupa 8/10.

2. Mbuyu Twite
Licha ya kadi nyekundu katika dakika za nyongeza , lakini jana kuna kitu nilikiona cha tofauti kidogo kwake. Mwanzoni walishindwa kuoana vyema na Msuva baada ya mshambuliaji huyo wa pembeni kucheza chini sana na kumfanya Twite kushindwa kuipa kasi yanga kutokea pembeni na kujikuta muda mwingi akicheza back passes na Yondani ama kucheza chini bila kuufungua uwanja hali iliyowafanya Simba hususani Kiiza kupata mwanya wa kuisogelea sana Yanga. Kutoka kwa Msuva kulianza kumuonesha Twite kama Compact wing back alikuwa anapanda na kushuka . Bado sio mzuri kwenye technical assist hasa kupiga krosi kama ambavyo hufanya Juma Abdul . Nakupa 7/10

3. Mwinyi Haji
Alikuwa vizuri kutimiza majukumu yake ila hakuwa bora katika kiwango chake. Ni mechi ya kwanza katika historia yake yenye ushindani mkubwa. Ushindani kimbinu, kiufundi na kisaikolojia. Mwanzoni alikosa utulivu na kubutua hovyo mipira . Mwinyi kiasilia ni kama kiungo mkabaji ana uwezo mkubwa kumiliki mpira na kuanzisha mashambulizi mazuri ya pembeni lakini pressure ilikuwa kubwa . Lakini baadae alitulia na kuanza kuifanya kazi yake vyema. Nakupa 7/10.

4. Nadir Haroub
Bado ni kiongozi ndani ya timu licha ya umri kuanza kuelekea magharibi ya soka. Dakika 18 za mwanzo alisimama kama Sweeper wa karne ya 20. " beki hasifiwi" falsafa ilitawala kichwa. Jinsi mpira ulivyokuja ndivyo alivyoubutua . Alisimama kama mtibuaji wa mwisho hakutaka masikhara lakini baaadae alitulia akishirikiana vyema na Yondani , Kamusoko na wing backs walianza kuipanga timu toka nyuma. Kuepusha ugomvi dakika ya 81 kulizidi kumuongezea credit kama nahodha . Nakupa 7/10.
5. Kelvin Yondani
Naweza sema ni moja ya mechi ambayo Cotton alikuwa ametulia na kuonesha ubora wake . Hakuwa na pressure na muda wote alionesha kujiamini sana . Rafu , ubabe vilipungua hakika ni mmoja ya wachezaji ambao waliibeba sana Yanga jana. Nakupa 8/10

Post a Comment