LEO Manchester United wako kwao Old Trafford kucheza Mechi ya Raundi ya 4 ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, dhidi ya Middlesbrough ambayo ipo Daraja la chini la Championship.
Baada ya kutoka Sare na CSKA Moscow, kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na Manchester City, kwenye Ligi Kuu England, Man United Leo wanapambana na Boro kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa Ligi Kuu England wa 2008/09 wakati Boro iliposhushwa Daraja.
Wakati Man United inatoka kwenye Sare, Boro wanatoka Mechi yao ya Ligi ambayo waliichapa Wolves 3-1 baada ya kuwa nyuma kwa Bao 1-0 na kushika Nafasi ya 4 katika Daraja la Championship.
Kwenye Mechi hii, Man United itawakosa Majeruhi Antonio Valencia, Luke Shaw and Paddy McNair, Ashley Young na James Wilson lakini ipo nafasi kubwa kwa Chipukizi kutoka Brazil, Andreas Pereira, akacheza hasa baada ya kuchezeshwa na kufunga Bao katika Mechi ya Raundi iliyopita ya Mashindano haya dhidi ya Ipswich Town.
Nae Meneja wa Boro, Aitor Karanka, amedokeza huenda akapumzisha Wachezaji wake kadhaa ili kutilia mkazo kwenye Ligi yao wakawania kupanda Daraja kurudi Ligi Kuu England.
Lakini, huenda Boro wakamtumia mkongwe Stewart Downing, ambae aliwahi kuichezea England, hasa baada ya Jumamosi kufunga Bao safi la Friki walipoichapa Wolves.
Refa wa Mechi hii atakuwa Lee Mason.
Capital One Cup
Raundi ya 4
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku ispokuwa inapotajwa
Jumanne Oktoba 27
Liverpool v Bournemouth
Manchester City v Crystal Palace
Southampton v Aston Villa
2300 Manchester United v Middlesbrough
Capital One Cup
Raundi ya 4
Matokeo:
Jumanne Oktoba 27
Everton 1 Norwich City 1 [Baada Dakika za Nyongeza 30, 1-1, Penati: Everton 4 Norwich 3]
Hull City 0 Leicester City 0 [Baada Dakika za Nyongeza 30, 1-1, Penati: Hull 5 Leicester 4]
Sheffield Wednesday 3 Arsenal 0
Stoke City 1 Chelsea 1 [Baada Dakika za Nyongeza 30, 1-1, Penati: Stoke 5 Chelsea 4]



Post a Comment