Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: FABRICIO COLOCCINI: NEWCASTLE YASHINDA RUFAA, KADI NYEKUNDU YAFUTWA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Newcastle United wameshinda Rufaa yao kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Beki wao Fabricio Coloccini wakati wanafungwa 3-0 na Sunderland k...

Newcastle United wameshinda Rufaa yao kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Beki wao Fabricio Coloccini wakati wanafungwa 3-0 na Sunderland kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Coloccini, mwenye Miaka 33, alitolewa kabla ya Haftaimu baada ya kumzuia Steven Fletcher kwenda kufunga na Refa kutoa Penati iliyowapa Sunderland Bao lao la kwanza.
Sasa Beki huyo yuko huru kucheza Mechi ya Newcastle ya Nyumbani kwao Saint James Park dhidi ya Stoke City ya Ligi Kuu England hapo Jumamosi.
Kutolewa nje kwa Coloccini ndiko kulikofungua njia kwa Sunderland kuitandika Newcastle Bao 3-0 kwenye Dabi ya Eneo la Wear-Tyne na hiyo ikawa mara ya 6 mfululizo kwa Sunderland kushinda Dabi hii.
Kipigo hicho kimeiacha Newcastle Nafasi ya 19 ya Ligi Kuu England wakiwa Pointi sawa na Sunderland lakini wao wako nyuma kwa Magoli.
Licha ya FA, Chama cha Soka England, kuikubali Rufaa ya Newcastle, Klabu hiyo sasa itajibu Mashitaka ya kushindwa kudhibiti Wachezaji wao kufuatia kumzonga Refa mara baada ya Coloccini kupewa Kadi Nyekundu.
Newcastle imepewa hadi Saa 3 Usiku, Saa za Bongo, hapo Ijumaa kujibu mashitaka hayo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top