Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: MKENYA OLUNGA AULA CHINA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Michael Olunga amejiunga na klabu iliopandishwa daraja katika ligi ya China Guizhou He...

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Michael Olunga amejiunga na klabu iliopandishwa daraja katika ligi ya China Guizhou HengFeng Zhicheng kwa kitita cha fedha kisizojulikana kutoka kwa klabu ya Djurgadens IF kutoka Sweden.

Olunga mwenye umri wa miaka 22 aliachiliwa na Djurgadens IF baada ya vilabu vyote viwili kukubaliana.

Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya, Olunga alikuwa amesalia na miaka mitatu katika kandarasi yake.

Mchezaji huyo wa zamani wa Gor Mahia na Tusker pia amekuwa akisakwa na klabu ya Urusi ya CSKA Moscow.

Guizhou Zhicheng Hengfeng ilikuwa imemuulizia mshambuliaji huyo na iliripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha shilingi milioni 467 zilizodaiwa na Djugardens.

Olunga pia alikuwa amevutia klabu ya Uturuki ya Galatasaray.

Mchezaji huyo aliifungia Gor Mahia mabao 19 katika msimu wa 2015, na kuwasaidia kushinda taji la 15 la KPL pamoja na taji la Top 8 kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Sweden.

source BBC

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top