Wakazi wa Mwakaleli juzi mkoani Mbeya walimstaajabisha kiungo mshambuliaji wa Mbeya City Mrisho Khalfan Ngasa kwa kumng'ang'ania wapige nae picha na kutia saini kwenye nguo zao kuonesha mapenzi makubwa kwa gwiji huyo wa soka nchini.
Timu ya Mbeya City imepiga kambi mjini Mwakaleli kujiandaa na mchezo wa jumamosi dhidi ya JKT Ruvu . Baada ya mazoezi yaliyokuwa yakishuhudiwa na wakazi hao , waliuvamia uwanja na kumkimbilia mchezaji huyo ambaye amepata kuvuma sana na mabingwa wa ligi kuu nchini Yanga SC pia akichagiza kipaji chake na Azam FC baadae Simba SC .
Ngasa anashikilia rekodi ya mfungaji bora kwa wachezaji walioko viwanjani hivi kwa timu ya taifa baada ya kutupia kwenye nyavu goli 25. Kipaji halisi , ucheshi na nidhamu yake inamfanya mchezaji huyo kuwa miongoni Mwa wachezaji wanaopendwa zaidi nchini licha ya kuanza kuisogelea magharibi ya soka lake.
Ngasa alianza kuingia kwenye soka la ushindani mwaka 2004 akiwa na Kagera Sugar na mwaka 2006 mabosi wa Jangwani wakamnasa na ndipo nyota yake ilipoanza kung'aa kitaifa.
Huyo ndio ANKOOL.............anasepa na kijiji.


Post a Comment