Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: 𝗬𝗔𝗡𝗚𝗔 𝗞𝗨𝗙𝗔𝗡𝗬𝗔 𝗠𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗢 𝗧𝗘𝗡𝗔.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari njema kwa mashabiki na wanachama wote wa 𝗬𝗮𝗻𝗴𝗮 ni kuwa Uongozi upo mbioni kutangaza mkutano na wananchama wao juu ya mchakato mz...
Habari njema kwa mashabiki na wanachama wote wa 𝗬𝗮𝗻𝗴𝗮 ni kuwa Uongozi upo mbioni kutangaza mkutano na wananchama wao juu ya mchakato mzima wa Mabadiliko. 

Kwa sasa unaweza kusema kama tayari taa ya kijani imeshawashwa kwa Uongozi wa Yanga kuanza utekelezaji wa rasimu ya mabadiliko kutoka La Liga kama washauri wao wa mchakato mzima wa mabadiliko. 

Mwenyekiti wa Yanga Dkt Msindo mbette msola na jopo lake lote la Uongozi litahitisha mkutano na wanachama wao kuwapa mrejesho mzima wa safari ya mabadiliko baada ya serikali kupitisha katiba mpya Yanga sc. 

𝗦𝗔𝗙𝗨 𝗬𝗔 𝗨𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗜 𝗞𝗨𝗦𝗨𝗞𝗪𝗔 𝗨𝗣𝗬𝗔

Katika Mfumo ambao Yanga wanaokwenda kuutumia kwa sasa kwenye mabadiliko ni mfumo ambao utakuwa na kiongozi mwenye cheo cha URAISI na MAKAMU WAKE Pamoja na CEO.Mfumo upoje….. 

Yanga itakwenda kuwa na wawekezaji wasiopungua wanne ambae kila mmoja wao atamiliki hisa asilimia 12.5% na kufanya jumla ya hisa 49% kumilikiwa na wawekezaji. Asilimia 51%zitakwenda kumilikiwa na Yanga wenyewe ambao wao watakuwa na kiongozi mwenye cheo cha CEO huku wawekezaji watakuwa na kiongozi mwenye cheo cha URAISI. 

Yanga watatoa wajumbe watano kwenda kwenye bodi na Wawekezaji watatoa wajumbe wanne ambao wataunda bodi yenye wajumbe 9 ila wenye maamuzi ya mwisho watakuwa ni Yanga ambao watakuwa na wajumbe watano. 

𝗞𝗟𝗔𝗕𝗨 𝗞𝗨𝗙𝗔𝗡𝗬𝗜𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗧𝗛𝗜𝗠𝗜(𝗧𝗛𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗟𝗜 𝗭𝗔𝗞𝗘)𝗞𝗔𝗕𝗟𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔𝗜𝗧𝗔 𝗪𝗔𝗪𝗘𝗞𝗘𝗭𝗔𝗝𝗜. 

Yanga ipo mbioni kumalizana na kampuni ambayo itakwenda kufanya tathimi ya mali zote za Yanga kuanzia majengo, wadhamini, mikataba ya wachezaji, usafiri(mabasi), nk kabla ya Uongozi wa 𝗬𝗮𝗻𝗴𝗮 kuwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza Yanga. 

𝗪𝗔𝗡𝗔𝗖𝗛𝗔𝗠𝗔 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗛𝗔𝗕𝗜𝗞𝗜 𝗞𝗨𝗦𝗔𝗝𝗜𝗟𝗜𝗪𝗔 𝗨𝗣𝗬𝗔 

Katika kuongeza tathamani ya klabu msingi mkubwa ambao Yanga watanufaika nao ni kujua idadi ya Wananchama na mashabiki kwa kuwasajili kwenye mfumo wa kisasa. Mchakato huu utafanyika Tanzania nzima na tayari baadhi ya mikoa Mwenyekiti ameshatembelea kutoa Elimu juu ya mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu yetu ya Yanga. 

𝗞𝗜𝗚𝗔𝗠𝗕𝗢𝗡𝗜 𝗖𝗢𝗠𝗣𝗟𝗘𝗫 "𝗛𝗢𝗠𝗘 𝗢𝗙 𝗖𝗛𝗔𝗠𝗣𝗜𝗢𝗡 "

Katika kuhakikisha Yanga inakuwa na miondombinu bora na ya kisasa Yanga itawakaribisha Wawekezaji kuja kuwekeza kwa kujenga viwanja viwili vya mazoezi kigamboni pamoja na hotel za wachezaji. Pia Yang itakwenda kunufaika kwa kuendesha academy ambayo itazalisha Wachezaji wengi wazawa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top