Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi ALMAS KASONGO amesema anashangaa kuona barua ndeeeeefu kutoka klabu ya SIMBA SSC ambayo hata Haina maudhui ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku akisema tayari walishawajibu Simba.
Mimi nashangaa sana hoja zinazotolewa za kupinga udhamini wa kampuni ya GSM, huku hoja zinazotolewa ni dhaifu na zimejikita kwenye ushabiki zaidi na SIYO weledi wa mambo ya soka--kasongo
Wakati TFF inahangaika kupata wadhamini wa ligi yetu watu hata hawana habari na hayawahusu tu ligi ikikosa wadhamini na baadhi ya timu zianze kushindwa kusafiri wao kwao furaha eti kwakuwa wapo na mtu anayewapa Kila kitu basi hawataki hata kujiuliza timu zingine zinasafirije posho za waamuzi pia siyo jukumu lao---kasongo
NBC na GSM hawajajileta wenyewe wametafutwa tena Kwa nguvu kubwa na ushawishi Leo hii mtu kakubali kuweka pesa zake unaanza vijimaneno visivyo na kichwa Wala miguu nadhani siyo sahihi na huu mkataba unahusu GSM na TFF hivyo kuujadili ni kosa pia kuuhoji siyo sahihi kwani unahusu pande mbili utauhoji vipi ikiwa haukuhusu na hujatoa hata mia--- KASONGO
Makampuni mengine yaliyoombwa kudhamini hata barua tu hawakuzijibu huwezi kumlazimisha mtu au kampuni itoe Hela na majina ya makampuni ambayo hata kujibu tu barua hayajajibu tunayo majina wengine ni wadau wa soka lakini hatuwezi kuyasema---kasongo
Ligi yetu Bado inahitaji pesa acheni hoja dhaifu leteni Hela ndiyo muwe na haki ya kuongea siyo vijimaneno vya kipuuzi tu huku mkinufaika na hali mbaya ya uchumi wa vilabu vingine siyo sawa hata kidogo---- alimalizia KASONGO
Post a Comment