Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: USIJE SEMA SIJAKWAMBIA...
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kwenye mashindano ya mbio za Magari za Langalanga mchuano ni mkali ile mbaaya na sio wa kukosa kwenye mbio ya mwisho. Miamba miwili inayochu...



Kwenye mashindano ya mbio za Magari za Langalanga mchuano ni mkali ile mbaaya na sio wa kukosa kwenye mbio ya mwisho.

Miamba miwili inayochuana Max Verstappen ambae yupo chini ya Redbull na Lewis Hamilton ambae yupo chini  ya Mercedes wote wamekusanya pointi sawa mpaka sasa yaani pointi 369.5 kila mmoja huku Mbio kwa mwaka huu ikiwa imesalia moja tu inayotarajiwa kupigwa Abu Dhabi wikiendi hii.

Jana Hamilton aliibuka na malalamiko kuwa Mpinzani wake kwa mwaka huu Max Verstappen anaendesha Gari huku akivunja Sheria mara kwa mara, lakini malalamiko yake hayo yalitupiliwa mbali na kutakiwa awekeze akili yake kwenye mbio za mwisho.

Ikumbukwe mara ya mwisho Redbull kuibuka na ushindi kwenye constructors ilikuwa ni mwaka 2013 ambapo walikuwa wanatumia engine machine ya Renault, lakini kwa sasa wanatumia machine ya Honda ambayo mara ya mwisho waliibuka kidedea mwaka 1991.

Nani ataibuka bingwa kati ya Lewis na Max?!
na je ni injini gani itaibuka kinara mwaka huu 2021?!

Endelea kufuatilia maandiko yangu...

@gang_chomba🇰🇪

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top