#repost @wastara24
__
Ikiwa bado mjadala kuhusu mkataba wa TFF na GSM ukiendelea kuwa gumzo nimepata kumtafuta mwanasheria aliyebobea kwenye masuala ya mikataba kujua hili jambo kisheria limekaaje
Nanukuu
📌Hili jambo ukiangalaia kimapana zaidi linachukuliwa kisiasa na si kisoka, ukiangalia kwa mapana na sheria zilivyo TFF ndiyo wenye ligi na sheria inawabeba kuingia mikataba na wadhamini
📌GSM ameweka 2.1 Bilion kwa miaka 2, NBC wameweka 2.5 B kwa miaka 3, hatufahamu vyote vilivyomo kwenye mkataba ila kwa fedha hiyo anahaki ya kukaa kwenye jezi kama makubaliano ya mkataba yanasema hivyo.
📌Content za Contract zinawabind TFF na GSM pekee, unatakiwa uwe sehemu ya mkataba ndiyo uweze kuhoji kuhusiana na mkataba husika
📌hakuna haja ya TPLB kuziita klabu kila inapotaka kuingia mikataba, klabu zimeuamini uongozi ndiyo maana wamewaweka pale, ukiangalia hata klabu za wanachama huwa wanaingia mikataba bila kuwaita wanachama wao, ila baada ya mkataba ndiyo utaona wanachama wanatangaziwa.
📌Mfano CAF wanadhaminiwa na Total kuna klabu yeyote iliwahi kuhoji mkataba huo? Badala yake klabu zinalazimika kubadili jersey na kuwaacha baadhi ya wadhamini wao na kuvaa wadhamini wa CAF
📌TFF wapongezwe katika hili miaka ya nyuma tuliona klabu zikishindwa kisafiri na nyingine zikishuka daraja kutokana na Ukata lakini sasa ni tofauti tunaona ushindani, klabu zingekuwa na hoja ya msingi kama wasingepata mgao wa fedha ambazo TFF wameingia mkataba.
📌Na kama issue ni upangaji matokeo na fair competition mamlaka zipo klabu zinazofanya hivyo zichukuliwe hatua hata kama mkataba usingesainiwa hili la upangaji matokeo halikubaliki . MWISHO WA KUNUKUU
Lakini ukirejea kwa upande wa klabu zinahoja ya msingi kwasababu jersey ni mali ya klabu si ya Shirikisho.
Klabu nyingi ulimwenguni kwa sasa wanategemea uuzaji wa jersey ili kuongeza kipato kwanza kwa kuuza kwa mashabiki pili kiweka matangazo ya makampuni na ukiangalia klabu nyingi kubwa ndiyo zimekuwa na wadhamini wengi kutokana na mauzo makubwa ya Jersey
UCL wao wanakaa kwenye bega tu na matangazo yao yote yanakaa kwenye mabango.
Kama klabu zinajidhatiti kwenda kwenye mabadiliko chakubadili kwanza ni kanuni na sheria na taratibu .
Post a Comment