Fundi wa soka kutoka nchini Uganda ambaye ndie mchezaji anaetajwa kuwa hatari kuelekea mechi ya watani wa jadi Tanzania bara tarehe 11 Disemba 2021.
Aucho mzaliwa wa Jinja nchini Uganda mwenye umri wa miaka 28, ndio injini ya Yanga SC eneo la kiungo. Ndio mlinzi wa Nabi katika patterns zake zote za kujilinda na kushambulia akiamua wanajangwani hao wacheze vipi .
Ni aina ya viungo wakabaji wa kisasa wenye uwezo mzuri kujenga mfumo mzuri wa timu kujilinda kwa kushambulia pia kuipa balansi timu katika kujenga mashambulizi yenye ujazo mzuri kwenye box ( numerical superiority) .
Wakati anakua kisoka, alikuwa anamuhusu vyema kiungo wa Ufaransa Patrick Viera hususani katika pasi zake za mwisho na uwezo wa kupambana ndani ya box la kati na wapinzani ( tactical dueling ).
Ni dhahiri mbinu za kocha wa Simba SC katika kuimiliki mechi ya Jumamosi , zinaanzia kwa huyu mwamba. Namna gani anaweza kuwajenga kimbinu kina Mkude, Bwalya , Mzamiru , Kanoute, Duncan , Lwanga na Morrison kucheza vyema mbele ya Doctor Aucho .
“ kama kocha wetu ataingia na approach nzuri ya kuhakikisha Aucho anakosa nafasi ya kuijengea Yanga mfumo bora wa kujilinda na kushambulia, wale wetu . Yule ndio mchawi wao pale kati . Mukoko tayari tunamjua ila Aucho ana akili sana katika kunyumbuka hususani akiwa na Bangala “ - shabiki wa Simba SC.
Aucho mwenyewe kuelekea mechi anasema , “ ni mechi yenye pressure ya matokeo kwa mashabiki wetu na kila mmoja wetu . Kikubwa kwa wale watakaopata nafasi kucheza, kucheza kwa utulivu ili kuondoa pressure na panic , inshaalah Allah anaweza kujalia matokea mema kwetu “ - Aucho.
“ nikiona sijui niupeleke wapi mpira humpa yeye na yeye hujua nini cha kufanya . Mbali ya makocha wangu kunijengea vingi lakini pia kaka mkubwa always ananiambia be calm hata kwenye hatari. Najifunza mengi kwake ingawa mimi ni mlinzi “ - Mwamnyeto
Samuel Samuel
Post a Comment