Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: MKWASA ATOA NENO KUELEKEA KARIAKOO DERBY
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Charles Boniface Mkwasa kocha mkuu Ruvu Shooting, ametoa maoni yake kuelekea mtanange wa watani wa jadi jioni ya leo jiji Dar es Salaam.  A...


Charles Boniface Mkwasa kocha mkuu Ruvu Shooting, ametoa maoni yake kuelekea mtanange wa watani wa jadi jioni ya leo jiji Dar es Salaam. 

Akielezea mechi hiyo inayozikutanisha Simba SC na Yanga SC, Mkwasa amesema itakuwa mechi ngumu yenye ushindani mkubwa.

“ timu zote zina vikosi vizuri na tukumbuke hizi mechi huwa haziangalii rekodi za michezo miwili mitatu nyuma kabla ya mechi . Kila derby ina joto lake . Hakuna wa kujipa uhakika wa kushinda mechi kabla ya dakika 90. Lakini kwa maoni yangu.. mechi ya leo, atakayepata goli mwanzo anaweza kujipa nafasi kubwa ya kushinda “ - Charles Boniface Mkwasa .

Mkwasa amepata kuvuma na Yanga SC kama kiungo tegemeo kwa miaka 10 mfululizo mpaka kustaafu pia kwa nyakati tofauti amekuwa kocha mkuu na msaidizi wa wanajangwami hao ambao leo wanakuatana uso kwa uso na mnyama Simba SC .

Boniface amegoma kabisa kutoa utabiri wake kwa nani kuibuka mshindi katika mechi hiyo licha ya Yanga SC kuonekana kujiamini zaidi kuibuka mshindi katika mechi ya leo.

“ soka ni mchezo wa mbinu, ufundi na bahati kulingana na mazingira ya mchezo husika. Huwezi kuipa timu asilimia 100% za kushinda ilihali anakutana na mpinzani wa level yake pia mwenye kikosi kizuri . Lakini pia duniani kote derby huwa na pressure yake ya tofauti ambayo kwa namna moja ama nyingine huwa na athari aidha chanya au hasi kwa timu husika. “ aliongeza kocha huyo mkongwe katika tasnia ya soka nchini akikinoa kikosi cha Ruvu Shooting kwa sasa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top