Ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Leeds United, umemfanya Pep Guardiola kufikisha mabao 500+ ya ligi kuu tangu ajiunge na Manchester City mwaka 2016.
Rekodi za Pep
🏟️ - 207 Mechi
✔️ - 153 Ushindi
✍🏿 - 25 Sare
✖️ - 29 Vichapo
🏆 - 3 Mataji ya ligi kuu
⚽ - 506 Mabao ya kufunga
🎯 - 165 Mabao ya kufungwa
Anakuwa kocha aliyefikisha mabao 500 kwa haraka zaidi katika historia ya ligi kuu ya England:
1 - Pep Guardiola (207 Mechi)
2 - Jurgen Klopp (234 Mechi)
3 - Alex Ferguson (265 Mechi)
4 - Arsene Wenger (271 Mechi)
5 - Joss Mourinho (289 Mechi)
Zaidi ya hapo, Manchester City imekuwa timu ya kwanza kufikisha haraka zaidi mabao 500 chini ya kocha mmoja.
Lakini hiyo inakuja baada ya matumizi makubwa ya fedha za masheikh wa kiarabu.
Pep ametumia zaidi ya pauni milioni 900 ambazo ni zaidi ya matrilioni ya shilingi za Tanzania.
Je, mafanikio yake yanatokana na uwezo mkubwa alionao au fedha nyingi anazotumia?
By Zakazakazi
Post a Comment